Pata taarifa kuu
ERITREA-ETHIOPIA-USHIRIKIANO

Rais wa Eritrea kuzuru Ethiopia

Rais wa Eritrea Isaias Afwerki (kushoto) na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed (kulia).
Rais wa Eritrea Isaias Afwerki (kushoto) na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed (kulia). REUTERS/GHIDEON MUSA ARON VISAFRIC

Rais wa Eritrea Isaias Afwerki atazuru Ethiopia siku ya Jumamosi, Waziri wa Eritrea wa Habari Yemane Meskel ametangaza leo Ijumaa. Ziara hii ya rais wa Eritrea nchini Ethiopia ni hatua mpya katika kuboresha maridhiano kati ya nchi hizo mbili, jambo ambalo limekaribishwa na nchi nyingi.

Matangazo ya kibiashara

Maridhiano haya yamemaliza miaka ya 20 ya vita kati nchi hizi mbili jirani za pembe la Afrika.

Ziara ya Rais wa Eritrea nchini Ethiopia inakujachini ya wiki baada ya ziara ya kihistoria ya Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed mjini Asmara, mji mkuu wa Eritrea.

Baada ya kutia saini kwenye "tamko la pamoja la amani na urafiki", Ethiopia na Eritrea zilitangaza wiki hii kuwa watafungua balozi zao na barabara zinazounganisha nchi hizo, kuanzisha upya safari za ndege kati ya nchi hizo mbili na kuimarisha maendeleo ya bandari zao.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.