Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-SIASA-USALAMA

Upinzani wategemea waangalizi wa Afrika nchini Zimbabwe

Nelson Chamisa katika mkutano na waandishi wa habari huko Harare Julai 17, 2018.
Nelson Chamisa katika mkutano na waandishi wa habari huko Harare Julai 17, 2018. © AFP

Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe, Nelson Chamisa, ametoa wito kwa waangalizi kutoka Afrika kuhakikisha kuna kuepo na uwazi katika uchaguzi mkuu wa Julai 30.

Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huo utakua wa kwanza tangu kuanguka kwa utawala wa Robert Mugabe mnamo mwezi Novemba mwaka jana.

Hata hivyo Bw Chamisa amefutilia mbali amehakikisha kwamba chama chake hakina nia yoyote yakususia uchaguzi licha ya hofu ya udanganyifu.

Umoja wa Afrika (AU) na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) wametuma waangalizi wake uchaguzi nchini Zimbabwe, ambapo uchaguzi wakati wa enzi za Mugabe uligubikwa mara nyingi na udanganyifu na vitisho.

Hivi karibuni rais wa sasa wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa, aliyekuwa makamu wa rais wa Robert Mugabe, aliahidi uchaguzi wa wazi na wa kuaminika. Lakini upinzani, unaokabiliwa na vitisho na wizi wa kura kutoka chama cha Zanu-PF, madarakani tangu uhuru wa Zimbabwe mwaka 1980, bado unashukua unaamini kuwa mambo hayo huenda yakatokea katika uchaguzi ujao.

Chama cha Movement for Democratic Change (MDC) cha Nelson Chamisa tayari kimeshutumu ukosefu wa uwazi katika uchapishaji wa kadi za kupigia kura, wakiomba ukaguzi huru wa orodha ya wapiga kura na kushutumu vyombo vya habari vinavyoshabikia chama tawala.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.