Pata taarifa kuu
MALI-UCHAGUZI-SIASA

Wananchi wa Mali kumchagua rais wao mpya Jumapili

Raia hawa wakimtazama Rais Ibrahim Boubacar Keïta akitangaza kwamba atawania katika uchaguzi wa urais (picha ya kumbukumbu).
Raia hawa wakimtazama Rais Ibrahim Boubacar Keïta akitangaza kwamba atawania katika uchaguzi wa urais (picha ya kumbukumbu). Michele CATTANI / AFP

Zaidi ya wapiga kura milioni nane wanatarajia kupiga kura siku ya Jumapili nchini Mali kumchagua rais wao mpya. Wagombea katika kinyang'anyiro hiki ni 24, ikiwa ni pamoja na rais anayemaliza muda wake Ibrahim Boubacar Keïta, na washindani wake 23 ikiwa ni pamoja na kiongozi wa upinzani Soumaila Cissé.

Matangazo ya kibiashara

Jumuiya ya kimataifa ambayo jeshi lake (Minusma) na lile la Ufaransa la (Barkhane) wanasubiri kwa uchaguzi huo uzinduzi mpya wa utekelezwaji wa mkataba wa amani uliotiliwa saini kuanzia mwezi Mei hadi Juni mwaka 2015 kati ya serikali na kundi la waasi wa zamani, lenye watu wengi kutoka jamii ya Tuareg, utekelezwaji ambao umechelewa kabisa.

Licha ya machafuko yanayosababishwa na makundi ya wanamgambo wa Kiislamu, ambayo si tu yamekua sugu, lakini yamesambaa kutoka kaskazini hadi katikati na kusini mwa nchi hiyo, katika hali ya hatari bila kusimama tangu mwezi Novemba mwaka 2015. Machafuko ambayo pia yanaripotiwa nchini Burkina Faso na nchi jirani ya Niger.

Matokeo ya kwanza yanatarajiwa kutangazwa ndani ya masaa 48, matokeo rasmi yatatangazwa Agosti 3. Na tarehe 12 Agosti, kutafanyika duru ya pili ya uchaguzi kama hakutapatikana msindi katika duru ya kwanza.

Kiongozi mkuu wa upinzani Soumaïla Cissé wakati wa mkutano wake huko Koulikoro, Julai 12, 2018.
Kiongozi mkuu wa upinzani Soumaïla Cissé wakati wa mkutano wake huko Koulikoro, Julai 12, 2018. Michele CATTANI / AFP

Rais anayemaliza muda wake Ibrahimu Boubacar Keita, aliye chaguliwa mnamo mwaka 2013 anapewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huo.

Kampeni ya uchaguzi ambayo itamalizika siku ya Ijumaa jioni iligubikwa na hali tata kuhusu orodha ya uchaguzi, ambapo upinzani ulishtumu kuepo kwa mpango wa kuiba kura.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.