Pata taarifa kuu
DRC-UFARANSA-UBELGIJI-USHIRIKIANO

Kinshasa yarejelea uamuzi wake kuhusu visa kwa Wafaransa na Wabelgiji

Rais wa DRC Joseph Kabila katika kikao maalum cha Bunge baada ya kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Augustin Matata, Novemba 15, 2016.
Rais wa DRC Joseph Kabila katika kikao maalum cha Bunge baada ya kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Augustin Matata, Novemba 15, 2016. © AFP

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imerejelea upya uamuzi wake wa awali kuhusu kutoa tu visa za kibinadamu au kwa sababu za afya kwa Wabelgiji na Wafaransa ambao wanataka kwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo “kwa zingatia mazungumzo yanayoendelea ikiwa ni pamoja na suala la visa”..

Matangazo ya kibiashara

Awali serikali ya DRC  kupitia Waziri wa Mambo ya Nje wa DRC Emmanuel Ilunga, ilizitaka balozi zake kutoa tu visa za kibinadamu au kwa sababu za matibabu kwa wananchi wa Ufaransa na Ubelgiji ambao wanataka kwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ikisema ni kulipiza kisasi kwa kufungwa kwa ubalozi wa Ulaya nchini humo.

Hatua hii ya kufuta uamuzi huo imechukulia saa chache baada ya kutangzwa hatua hiyo ya mwanzo.

"Kwa kuzingatia mazungumzo yanayoendelea ikiwa ni pamoja na suala hili la visa, uamuzi kuhusu usawa umefutwa," kulingana na ujumbe mpya kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje Emmanuel Ilunga.

Awali Bw Ilunga aliandika "ni dhahiri kwamba balozi za Ubelgiji na Ufaransa wanatoa tu visa za kibinadamu au kwa sababu za matibabu kwa wananchi wa DRC tangu kufungwa kwa Ofisi ya Schengen.

"Balozi zetu zote zimetakiwa kutekeleza masharti haya kwa kulipiza kisasi na na kanuni ya usawa," Bw Ilunga aliongeza.

Ubalozi wa Ulaya unaosimamiwa na Ubelgiji, Ofisi ya Schengen, ilifungwa tangu mwanzoni mwa mwaka huu kwa ombi la serikali ya DRC. Ofisi hiyo ilikua ikishughulikia maombi ya visa kwa nchi 18 za Ulaya.

Kufungwa kwa ofisi ya Schengen ilikuwa moja ya hatua zilizotangazwa na serikali ya Kinshasa baada ya Ubelgiji kuikosoa wa serikali ya rais Kabila.

Hivi karibuni Ufaransa iliitolea wito serikali ya DRC "kufufua" mazungumzo na jumuiya ya kimataifa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.