Pata taarifa kuu
MALI-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Kiongozi wa upinzani aahidi kuboresha amani nchini Mali

Kiongozi wa upinzani nchini Mali, Soumaïla Cissé, katika kampeni yake ya uchaguzi huko Mopti, katikati mwa Mali, Julai 26, 2018.
Kiongozi wa upinzani nchini Mali, Soumaïla Cissé, katika kampeni yake ya uchaguzi huko Mopti, katikati mwa Mali, Julai 26, 2018. Twitter/ Soumaïla Cissé

Kiongozi wa upinzani nchini Mali, Soumaila Cisse, katika kampeni yake ya uchaguzi mjini Mopti (katikati mwa Mali), ameahidi kuboresha "amani" katika nchi hiyo ambapo machafuko ya kikabila yameongezeka kwa miaka mitatu.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na Idhaa hii, kiongozi wa upinzani Soumaila Cisse, amesema muda umefika kuwepo na jitihada za kuboresha amani katika nchi hiyo.

Upizani nchini Mali umependekeza kukutana na waziri mkuu wa nchi hiyo kuelekea Uchaguzi wa urais siku ya Jumapili, ambapo wanasiasa hao wamekuwa wakilalamikia kuwepo dalili za kufanyika kwa udanganyifu wa kura.

Waangalizi wa Uchaguzi wa urais nchini Mali utakaofanyika siku ya Jumapili wanasema, zoezi hilo litakuwa kipimo cha uthabiti wa nchi hiyo.

Wagombea 24 wanawania nafasi hiyo, akiwemo rais wa sasa Ibrahim Boubacar Keita, ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2013.

Mpinzani wake wa karibu ni Soumaila Cisse ambaye anatarajiwa kuleta upinzani katika uchaguzi huo ambao pia utapima hali ya usalama ya nchi hiyo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.