Pata taarifa kuu
MALI-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Wananchi waendelea kusubiri matokeo ya uchaguzi Mali

Cécile Kyenge, mkuu wa ujumbe wa waangalizi wa Umoja wa Ulaya wakati wa zoezi la kuhesabu kura huko Bamako, Julai 29, 2018.
Cécile Kyenge, mkuu wa ujumbe wa waangalizi wa Umoja wa Ulaya wakati wa zoezi la kuhesabu kura huko Bamako, Julai 29, 2018. REUTERS/Luc Gnago

Baada ya kushiriki katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais Jumapili, Julai 29, wananchi wa Mali wanaendelea kusubiri matokeo ya uchaguzi huo. Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya usalama ba kidiplomasia, vituo vya kupigia kura vilifungwa saa 12 jioni saa za kimataifa (sawa na saa mbili usiku saa za Afrika ya Kati).

Matangazo ya kibiashara

Rais anayemaliza muda wake, Ibrahim Boubacar Keïta, alipambana katika uchaguzi huo na wagombea wengine 23, ikiwa ni pamoja na kiongozi wa upinzani Soumaïla Cissé. Uchaguzi ulifanyika katika hali ya kawaida katika miji mikubwa ya nchi. Hata hivyo baadhi ya matatizo yalishuhudiwa katikati na kaskazini mwa Mali.

Zaidi ya raia milioni nane nchini Mali walipiga kura katika uchaguzi muhimu kwa taifa hilo la Sahel ambalo limekabiliwa na usalama mdogo kutokana na mashambulizi kutoka kwa makundi ya kijihadi.

Rais Keita amekuwa akikosolewa na wapinzani wake kwa kushindwa kurejesha usalama lakini na hata waliokuwa mawaziri wake walisema rais huyo ameshindwa kurejesha usalama.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Gutereres alisema anatiwa moyo na jinsi ambavyo kumekuwepo na amani wakati wa kampeni licha ya changamoto za usalama kwenye maeneo ya kaskazini na kati mwa taifa hilo la Mali.

Katika vituo vingi vya kupigia kura, wapiga kura wengii walizuiwa kupiga kura kwa sababu kadi zao za kupiga kura hazikupatikana katika vituo vya kupigia kura kwa ukiukwaji mkubwa wa sheria, au kwa sababu ya kukosa vifaa vya uchaguzi, Tiébilé Dramé, msemaji Soumaïla Cissé ameshtumu.

Huenda hii ni sehemu ya mchakato ambao utachukua muda mwingi. Mali inazaidi ya kilomita za mraba milioni mmoja, mfumo wa mawasiliano ni mbaya, hasa wakati huu wa msimu wa mvua.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.