Pata taarifa kuu
SOMALIA-AL SHABAB-UGAIDI

Al Shabab yadai kuwauwa wanaume watano hadharani

Magaidi wa Al Shabab
Magaidi wa Al Shabab wikipedia

Kundi la kigaidi la Al Shabab nchini Somalia linasema limewauwa wanaume watano, watatu kutoka Marekani akiwemo mmoja kutoka Uingereza.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa, kundi hili lilichukua hatua hii kwa madai kuwa watu hao walikuwa wanafanya kazi ya inteljensia kwa niaba ya serikali ya Mogadishu.

Watu hao waliuawa kwa kupigwa risasi hadharani siku ya Jumanne katika eneo ambalo linadhibitiwa na magaidi hao.

Mataifa ya Marekani na Uingereza hayajazungumzia madaia haya.

Hii sio mara ya kwanza kwa kundi la Al Shabab kudai kutekeleza mauaji kama haya.

Mwaka 2017, magaidi wa Al Shabab, walituhumiwa kuwauwa wanaume watano akiwemo mvulana mmoja kwa madai ya kufanya kazi kwa niaba ya serikali za Kenya na Marekani.

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.