Pata taarifa kuu
SOMALIA-MAREKANI-USALAMA

Marekani yadai kuua magaidi 60 nchini Somalia

Askari akiwa katika eneo la la shambulizi dhidi ya msafara wa ujumbe wa Umoja wa Ulaya, Mogadishu,  Somalia, 1 Oktoba 2018.
Askari akiwa katika eneo la la shambulizi dhidi ya msafara wa ujumbe wa Umoja wa Ulaya, Mogadishu, Somalia, 1 Oktoba 2018. REUTERS/Feisal Omar

Marekani imesema mashambulizi ya angaa yaliyotekelezwa na ndege zake za kivita nchini Somalia, yamesababisha vifo vya watu 60. Lakini taarifa hii haijashibitishwa na serikali ya Somalia, wala kukanushwa na kundi la Al Shabab.

Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Ulinzi nchini Marekani imesema haya yamekuwa mashambulizi makubwa kuwahi kutekelezwa na wanajeshi wake nchini Somalia kwa karibu kipindi cha miaka miwili.

Mwaka 2017, mashambulizi mengine kama haya yalifanyika na kusababisha mauaji ya magaidi 100 wa Al Shabab walipokuwa wanafanya mazoezi.

Mashambulizi ya hivi punde, yametokea katika eneo la Pwani la Harardhere , mafanikio ambayo yamekuja kwa ushirikiano wa wanajeshi wa Umoja wa Afrika AMISOM na wale wa Somalia.

Siku za hivi karibuni, mashambulizi ya angaa dhidi ya Al Shabab yameongezeka, lengo likiwa ni kuwamaliza nguvu magaidi hao ambao bado wanasalia kuwa hatari kwa usalama wa Somalia na ukanda wa Afrika Mashariki.

Mwaka uliopita, rais Donald Trump aliwaagiza wanajeshi wake kutekeleza mashambulizi dhidi ya magaidi wa Al Shabab, aliosema ni hatari kwa usalama wa dunia na washirika wake.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.