Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-SIASA-USALAMA

Ethiopia yampata rais mpya mwanamke

Rais mteule aw Ethiopia Sahle-Kazi Zewde, akula kiapo mbele ya Bunge, Addis Ababa, Oktoba 25, 2018.
Rais mteule aw Ethiopia Sahle-Kazi Zewde, akula kiapo mbele ya Bunge, Addis Ababa, Oktoba 25, 2018. © AFP

Wabunge wa Ethiopia wamechaguwa kwa pamoja, kwa mara ya kwanza, mwanamke, Sahle-Kazi Zewde, kuwa rais wa nchi hiyo, baada ya mtangulizi wake kujiuzulu kwenye nafasi hiyo ya heshima.

Matangazo ya kibiashara

Sahle-Work mwanadiplomasia, mwenye umri wa miaka 68, anakuwa rais wa nne nchini Ethiopia tangu kupitishwa kwa katiba ya mwaka 1995. Katiba hii inasema kuwa rais anaweza kuchaguliwa ikizidi sana mara mbili kwa mihula miwili ya miaka sita.

Sahle-Work, hadi kabla ya kuchaguliwa kwake alikuwa Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika Umoja wa Afrika (AU). Hapo awali, alikuwa balozi wa Ethiopia nchini Ufaransa, Djibouti, Senegal, na Mwakilishi wa Kudumu wa Ethiopia katika Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Afrika mashariki (IGAD).

Sahle-Work, ambaye alizaliwa Addis Ababa na ambaye alisomea nchini Ufaransa, sasa ni rais pekee mwanamke barani Afrika.

Wakati wa hotuba yake ya kuapishwa, amekaribisha mageuzi yaliyofanywa na Waziri Mkuu mpya Ahmed Abiy, ambaye alichukua madaraka mnamo mwezi Aprili.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.