Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-UFARANSA-USHIRIKIANO

Macron aipongeza Ethiopia kwa mageuzi chanya

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kulia) katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed (kushoto), baada ya mkutano wao katika ikulu ElyseeJumatatu, Oktoba 29, 2018, Paris.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kulia) katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed (kushoto), baada ya mkutano wao katika ikulu ElyseeJumatatu, Oktoba 29, 2018, Paris. Michel Euler / POOL / AFP

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amempongeza Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kwa mageuzi chanya ambayo amefanya, na ametangaza kwamba atazuru Ethiopia mwezi Machi.

Matangazo ya kibiashara

"Kwa chochote kile ambacho Ufaransa unaweza kufanya chenye manufaa, utakifanya" ili "kusaidia marekebisho" yanayofanywa na Bw Abiy, mwenye umri wa miaka 42, tangu kuchukuwa madaraka mnamo mwezi Aprili. Bw Abiy aliwaachilia huru maelfu ya wafungwa ikiwa ni pamoja na wanasiasa wa upinzani na waasi, alitia saini kwenye mkataba wa amani na jirani yake Eritrea na kutangaza kubinafsisha makampuni makubwa ya umma.

"Najua ni kiasi gani alijiingiza hatarini," alisema Emmanuel Macron wakati akimpokea Bw Abiy katika ikulu ya Elysee. Ahmed Abiy ambaye anafanya ziara yake ya kwanza barani Ulaya, anatarajia kuendelea na ziara yake leo Jumanne nchini Ujerumani.

Rais wa Ufaransa ameelezea nia yake ya kuzuru Ethiopia "kwa siku kadhaa". Ethiopia ni nchi ya pili yenye idadi kubwa zaidi ya watu barani Afrika yenye wakazi milioni 105.

Abiy amesema kuwa mapigano ya kikabila ambayo yameongezeka katika miezi ya hivi karibuni "hayawezi kuathiri mchakato wa mageuzi" kwa sababu " mchakato huo unaendeshwa na wananchi wa Ethiopia."

Karibu watu milioni moja walilazimika kutoroka makazi yao baada ya mapigano kati ya watu kutoka jami Oromo na jamii ya watu wachache ya Gedeo kusini mwa nchi. Mapigano ambayo yalizuka baada ya kuteuliwa kwake.

Katika ziara yake nchini Ufaransa, Ahmed Abiy na Emmanuel Macron walitia saini kwenye mikataba kadhaa ya ushirikiano kwa "kusaidia mchakato wa mageuzi ya Ethiopia" katika nyanja ya uchukuzi, nishati na utamaduni.

Emmanuel Macron pia alimpongeza Sahle-Kazi Zewde, aliyechaguliwa kuwa rais wa Ethiopia siku ya Alhamisi, akiwa ni mwanamke wa kwanza kuchukua nafasi hii nchini Ethiopia.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.