Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-JAMII-USALAMA

Ethiopia yakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kikabila

Familia ya watu kutoka kabila ya Oromo katika kambi ya wakimbizi ya Adama, Ethiopia, Oktoba 4, 2017 (picha ya kumbukumbu).
Familia ya watu kutoka kabila ya Oromo katika kambi ya wakimbizi ya Adama, Ethiopia, Oktoba 4, 2017 (picha ya kumbukumbu). © Paul Schemm / AFP

Mapigano ya mara kwa mara kwenye mpaka kati ya mkoa wa Oromia na eneo la Benishangul-Gumuz upande wa magharibi mwa Ethiopia yanaendelea kwa miezi miwili sasa. Hali hiyo imesababisha watu wengi kupoteza maisha na wengine kulazimika kutoroka makazi yao na kukimbilia katika maeneo salama.

Matangazo ya kibiashara

Mamlaka inajaribu kukabiliana na hali hiyo lakini imeshindwa, kwa mujibu wa chanzo cha serikali ambacho hakikutaja jina lake.

Hata hivyo Waziri Mkuu wa sasa Abiy Ahmed amefanikiwa pale ambapo wengi walishindwa. Waziri Mkuu huyo alitia saini kwenye mkataba wa amani na nchi jirani ya Eritrea na makundi kadhaa ya upinzani.

Lakini mgogoro wa kikabila unaendelea kuchafua utawala wake. Tangu mwezi Januari, Ethiopia imeorodhjesha watu milioni moja na nusu waliotoroka makazi yao kutokana na mchafuko ya kikabila.

Kwa mujibu wa mtafiti, mfumo wa utawala wa Ethiopia, uliojengwa kwa msingi wa kikabila, ulifaulu kupitia serikali kuu, hasa wakati wa Waziri Mkuu Meles Zenawi, aliyefariki dunia mwaka 2012.

Tangu wakati huo, mfumo huo uligeuka, na matokeo yake sasa yameanza kujitokeza hasa kwa madai ya walio wachache. Kwa mujibu wa mtaalam mmoja, makundi ya waasi yaliyorejea nchini "baadhi yaliendelea kuishi na silaha zao, kwa misingi ya kikabila," amesema.

Katika mapigano yaliyotokea kwenye mpaka wa mikoa ya Oromia na Benishangul-Gumuz, mamlaka inasema kuwa watuhumiwa zaidi ya 200 wamekamatwa. Baraza la usalama la kitaifa limetangaza kwamba limetuma vikosi vya nchi hiyo kwenye mpaka wa mikoa hiyo miwili.

Waziri Mkuu mwenywe ni kutoka kabila la Oromo na ni kiongozi wa ODP. Chama tawala katika mkoa wa Oromia kilikutana katika kikao cha dharura mwishoni mwa wikina kushutumu kundi moja "kuchochea mauaji".

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.