Pata taarifa kuu
SUDAN-DARFUR-USALAMA

Darfur: Makundi mawili ya waasi na serikali ya Sudan wafikia makubaliano

Wapiganaji wa kundi la waasi la JEM (picha ya kumbukumbu).
Wapiganaji wa kundi la waasi la JEM (picha ya kumbukumbu). RFI/Stéphanie Braquehais

Makundi mawili hasimu ya waasi na serikali ya Sudan wametia saini kwenye makubaliano ya mazungumzo ya amani Darfur. Makubaliano hayo yamefikiwa siku ya Alhamisi wiki hii katika mji mkuu wa Ujerumani, Berlin.

Matangazo ya kibiashara

Makubaliano hayo yaliidhinishwa na makundi mawili ya waasi JEM na SLA-MM pamoja na Amin Hassan al Omari, mwenyekiti wa Mazungumzo kwa upande wa serikali ya Sudan.

Mazungumzo hayo yalifanyika chini ya mwamvuli wa Umoja wa Afrika, akiwepo rais wa zamani wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki, ambaye anaongoza ujumbe wa ngazi ya juu wa Umoja wa Afrika katika kushughulikia migogoro ya Sudan.

Mkataba huu ni hatua ya kwanza kuelekea mchakato mpya wa mazungumzo kati ya makundi tofauti katika mgogoro Darfur.

Mkataba huo unaandaa hatua zijazo. "Nadhani hatua iliyopigwa ni hatua muhimu katika kuendelea mambo, lakini hii hapa ni mwanzo tu," amesema Gibril Ibrahim, kiongozi wa kundi kuu la waasi la JEM.

"Tunataka kuwepo na nia nzuri ya kisiasa na bidii kwa kufikia amani Darfur. Mambo yanaendelea vizuri. Mjini Berlin, kulikuwa na shauku kubwa kati ya pande zinazohusika na wanachama wa jumuiya ya kimataifa, kwa kuendeleza mchakato wa amani kwa muda mfupi, " Bw Ibrahim ameongeza.

Kwa mujibu wa msemaji wa JEM, mkataba huu wa "nia nzuri" utafuatiwa na mwingine ambao utasitisha mapigano, na wa tatu ambao utatoa ratiba ya mazungumzo ya kukomesha vita vya tangu mwaka 2003 katika Sudan ya magharibi.

Umoja wa Afrika, ambao ni mpatanishi katika suala hili kwa miaka mitatu, ulifaulu kuzikutanisha pande mbalimbali katika mazungumzo bila masharti yoyote.

Kwa mujibu wa duru za kuaminika, mazungumzo mapya yatafanyika Januari 12, 2019.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.