Pata taarifa kuu
MISRI-USALAMA-HAKI

Misri yapiga marufu uuzaji wa vizibao vya njano

Vizibao vya njano vimekuwa ni tishio kwa maandamano kwa baadhi ya nchi za Afrika, hususan Misri.
Vizibao vya njano vimekuwa ni tishio kwa maandamano kwa baadhi ya nchi za Afrika, hususan Misri. Lucas BARIOULET / AFP

Mamlaka nchini Misri imezuia uuzaji wa vizibao vya njano, ambavyo vimekuwa ni ishara kwa maandamano ya kijamii nchini Ufaransa, na kwa sasa uuzaji wa bidhaa hiyo umewekwa chini ya udhibiti wa polisi, wafanyabiashara kadhaa wamelalamikia hali hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Wafanyabiashara watano wa Cairo wameliambia shirika la Habari la AFP kuwa uuzaji wa vizibao vya nyano hauwezekani bila idhini kutoka mamlaka husika.

Kwa mujibu wa mmoja wa wafanyabiasha, "unapotaka kuuza vizibao vya ya njano, unatakiwa kupewa idhini na kituo cha polisi" katika eneo unakofanyia biashara.

Kwa mujibu wa mashahidi, baadhi ya wafanyabiasaha wanauza vizibao vya njano kwa siri, huku wakisema: fichika haraka! Kuuza bidhaa hii ni hatari zaidi kuliko kuuza madawa ya kulevya."

"Maafisa wa usalama wamekuja na kutuomba tusiuzi vizibao vya njano," amesema mfanyabiashara mwengine. "Wanaogopa nchii isikumbwe na maandamano baada ya yale yanayotokea Ufaransa".

Aidha, kwa mujibu wa mmoja wa waagizaji waliohojiwa na AFP, ambaye hakutaja jina lake, amri hiyo ilitolewa kwa makampuni yanayoagiza bidhaa hiyo kutoka nje ya nchi "juma lililopita" kwa kuuzia tu makampuni yanayojulikana na sio watu binafsi.

Wakati huo huo, siku ya Jumanne mahakama ya Misri iliamuru Mohamed Ramadan, mwanasheria anayejulikana kwa msimamo wake kuhusu haki za binadamu, azuiliwe kwa siku 15 kwa kosa la "tishio kwa usalama".

Mwanasheria huyo, aliyekamatwa siku ya Jumatatu kaskazini mwa Alexandria, anadaiwa kuchapisha kwenye umtandao wa Facebook ujumbe ambapo anaomba wakazi wa Alexandria, kununua vizibao vya njano, amesema mwanasheria wake Abdelrahman al-Gohary.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.