Pata taarifa kuu
SUDAN-MAANDAMANO-UCHUMI

Polisi yakabiliana na waandamanaji Sudan

Hali iliyoshuhudiwa wakati wa maandamano dhidi ya kupanda kwa bei ya bidhaa mahitajio hasa mkate katika mji wa Atbara, Sudan, Desemba 20, 2018.
Hali iliyoshuhudiwa wakati wa maandamano dhidi ya kupanda kwa bei ya bidhaa mahitajio hasa mkate katika mji wa Atbara, Sudan, Desemba 20, 2018. REUTERS/El tayeb Siddig

Maandamano mapya dhidi ya kuongezeka kwa bei ya mkate yameongezeka jana Jumapili nchini Sudan huku polisi wa kuzuia ghasia wakisambazwa kwenye mji mkuu wa Khartoum kwa siku tano za maandamano ambayo tayari yamegharimu maisha ya takribani watu nane.

Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji walichoma matairi na matawi ya miti mitaani na kujaribu kuharibu jengo la serikali kabla ya kuzuiwa na maafisa wa usalama, mashahidi alisema.

Viongozi wa upinzani nchini humo wanasema waandamanaji 22 wameuawa katika maandamani hayo yaliyoanza wiki iliyopita, kwa kupigwa risasi na polisi.

Polisi nchini Sudan wameendelea kukabiliana na waandamanaji katika miji mbalimbali.

Mamia ya waandamanaji jana, walikabiliana na polisi karibu na uwanja wa soka jijini Khartoum.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.