Pata taarifa kuu
DRC-AJALi-USALAMA

Ishirini na sita wafariki dunia katika ajali ya barabarani Kinshasa

Timu ya matabibu wakiwasili katika eneo la ajalii, Jumamosi 6 Oktoba, 2018.
Timu ya matabibu wakiwasili katika eneo la ajalii, Jumamosi 6 Oktoba, 2018. RFI / Patient Ligodi

Watu zaidi zaidi ya ishirini na tano, wamepoteza maisha nchini DRC, katika barabara ya kutoka jiji kuu la Kinshasa kwenda Matadi, Magharibi mwa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Ajali hii imetokea, wakati raia wa nchi hiyo wakisherehekea sikukuu ya Krismasi.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la AFP ambalo limefanya mahojiano na baadhi ya mashahidi linasema kuwa watu 27 ndio wamepoteza maisha katika ajali hiyo.

“Kumetokea ajali katika barabara ya kutoka jiji kuu la Kinshasa kwenda Matadi, mpaka sasa watu 26 ndio wamepoteza maisha," amesema Waziri miundombinu katika serikali ya mkoa wa Kongo ya Kati, Papy Mambo Luamba, ambaye alihojiwa na shirika la Habari la AFP.

Chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana lakini mashahidi wanasema gari hizo zilikuwa kwenye mwendo wa kasi.

Oktoba 6 zaidi ya watu hamsini walipoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa katika mji wa Mbuba karibu na Kisantu Baada ya lori moja lililokuwa limebebea mafuta kugongana na lori la mizigo.

Mpaka sasa haijajulikana idadi rasmi ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo ya Lori kugongana na basi.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya polisi katika mji jirani wa Kisantu, katika Congo ya Kati, idadi ya watu waliopoteza maisha inaweza kuongezeka.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.