Pata taarifa kuu
SUDAN-MAANDAMANO-UCHUMI

Mamia ya wafuasi wa Bashir waingia mitaani, maandamano ya upinzani yavunjwa

Maandamano ya kumuunga mkono Rais wa Sudan Omar al-Bashir mjini Khartoum, tarehe 9 Januari 2019.
Maandamano ya kumuunga mkono Rais wa Sudan Omar al-Bashir mjini Khartoum, tarehe 9 Januari 2019. © AFP

Mamia ya wafuasi wa Rais wa Sudan Omar al-Bashir wameandamana mjini Khartoum Jumatano wiki hii wakisema wanauunga mkono utawala wake, ambao ulikabiliwa na maandamano makubwa katika wiki za hivi karibuni.

Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo vikosi vya usalama vimetumia mabomu ya machozi kwa kutawanya mkusanyiko wa waandamanaji wanaopinga utawala nchini Sudan.

"Mkusanyiko huu unatuma ujumbe kwa wale wanaofikiri kuwa Sudan itaishia kama nchi nyingine zinazokumbwa na machafuko," Rais Omar al-Bashir, amesema huku akipongezwa na wafuasi wake.

"Tutamkamata mtu yeyote ambaye anataka kuharibu mali zetu," ameongeza.

Rais wa Sudan aliwasili kwenye eneo la mkutano katika bustani kubwa ya mji mkuu Khartoum ya Green Yard, huku akivalia suti na suruali ya rangi ya kahawia. Kabla ya kuanza kuzungumza, aliwasalimu wafuasi wake.

Watu wasiopungua 19, ikiwa ni pamoja na polisi wawili, waliuawa wakati wa maandamano, kwa mujibu wa serikali.

Hata hivyo shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International linasema waandamanaji 37 ndio waliuawa katika maandamano hayo yanayoendelea.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.