Pata taarifa kuu
AFRIKA-UN-CHINA-USALAMA-AMANI

Kanda ya Maziwa makuu yapata mwakilishi mpya wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Huang Xia, wakati alikuwa balozi wa China Senegal, hapa ilikuwa mnamo mwezi Aprili 2015.
Huang Xia, wakati alikuwa balozi wa China Senegal, hapa ilikuwa mnamo mwezi Aprili 2015. SEYLLOU / AFP

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amemteua balozi wa China, Huang Xia, kama mjumbe wake mpya katika eneo la Maziwa Makuu. Huang Xia anachukua nafasi ya Saïd Djinnit aliye kuwa mjumbe wa Antonio Guterres katika eneo hilo.

Matangazo ya kibiashara

Balozi wa zamani wa Niger, Senegal na Congo Brazzaville, Huang Xia, ambaye pia alikuwa balozi nchini Gabon na Ufaransa, anakuwa mjumbe maalumu wa kwanza kutoka China.

Uteuzi huu unaipa China kushikilia nafasi kubwa katika Umoja wa Mataifa. Hatua hii ya Katibu Mkuu wa Umoja aw Mataifa inaonyesha mchango mkubwa wa CHina katika umoja huo, kwa mujibu wa vyanzo vya kidiplomasia kutoka Umoja wa Mataifa ambavyo havikutaja majina yao.

"Huu ni mjumbe maalumu wa kwanza kutoka China," chanzo cha kidiplomasia cha China kimeliambia shirika la Habari la AFP, huku kikipongeza hatua hiyo ya Katibu Mkuu wa Umoja aw Mataifa Antonio Guterres.

China ambayo kwa sasa inaendelea kuimarisha uhusiano wake wa kidiplomasia barani Afrika, imekuwa mchangiaji mkubwa wa fedha kwa Umoja wa Mataifa baada ya Marekani, nafasi ambayo imekuwa ikishikiliwa na Japan.

China inachangia 12% ya bajeti ya Umoja wa Mataifa na 15% ya shughuli za amani za umoja huo.

China ambayo ni mwanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ilio na kura veto, pia ni mchangiaji mkubwa wa misaada ya Umoja wa Mataifa, na ina zaidi ya Walinda amani 2,500 waliotumwa nchini Mali, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Sudan Kusini na Lebanon.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.