Pata taarifa kuu
CAR-UN-USALAMA-VIKWAZO

Jamhuri ya Afrika ya Kati kukabiliwa na vikwazo kwa mwaka wa mwisho

Mtu mwenye silaha akitoa ulinzi katika eneo la PK5, Bangui, RCA, mnamo Novemba 15, 2017.
Mtu mwenye silaha akitoa ulinzi katika eneo la PK5, Bangui, RCA, mnamo Novemba 15, 2017. © AFP

Umoja wa Mataifa umetoa msamaha mpya kwa Urusi na China kwa kukiuka vikwazo vya silaha vilivyowekewa Jamhuri ya Afrika ya Kati. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajia kupitia upya na kuongeza vikwazo hivyo kwa mwaka mmoja siku ya Alhamisi, lakini labda ikawa mwaka wa mwisho wa vikwazo vya silaha kwa Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Matangazo ya kibiashara

Rasimu ya azimio ambayo imeandikwa na Ufaransa, inaeleza kwa mara ya kwanza "nia" ya Baraza la Usalama ya kupunguza vikwazo vya silaha vilivyowekwa tangu mwaka 2013 ifikapo Septemba 30, kutokana na hatua kubwa ya maendeleo katika suala la wa usalama nchini humo.

Kwa hivyo, vigezo vitawekwa na hatua ya mafanikio iliyoombwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres tarehe 31 Julai.

Mamlaka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambayo kwa muda mrefu wamekuwa wakiomba kufutiwa vikwazo vya silaha katika hali ya kukabiliana vilivyo na makundi ya watu wenye silaha ambayo yanadhibiti maeneo mengi ya nchi.

Vigezo muhimu na vilivyo bora vitawekwa wazi tarehe 30 Aprili kuhusu "mageuzi ya sekta ya usalama, kupokonya silaha watu wanaozimiliki kinyume cha sheria, kuwarejesha wapiganaji katika maisha ya kiraia na mchakato wa kuwaingiza wapiganaji katika jeshi na vikosi vya usalama.

Vyote hivyo vitawezesha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchunguza vikwazo vya silaha" mwishoni mwa mwezu Septemba, nakala hiyo imesema maandiko.

Siku ya Jumatatu, takriban watu 3,000, ikiwa ni pamoja na Waziri Mkuu Mathieu Simplice Sarandji, walisirika katika maandamano mjini Bangui kuomba tena tena kufutiwa vikwazo vya silaha.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.