Pata taarifa kuu
SOMALIA-USALAMA

Kumi na tatu waangamia katika shambulio Mogadishu

Shambulio la bomu lililotegwa katika gari laua watu kumi na kujeruhi zaidi ya 20 katika hoteli moja Mogadishu .
Shambulio la bomu lililotegwa katika gari laua watu kumi na kujeruhi zaidi ya 20 katika hoteli moja Mogadishu . REUTERS/Feisal Omar

Watu kumi na tatu wameuawa katika shambulio lililolenga hoteli moja katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu. Watu zaidi ya 20 wamejeruhiwa, majengo kadhaa ya eneo hilo linalotembelewa na watu wengi katikati mwa mji huo yameharibika, kwa mujibu wa polisi.

Matangazo ya kibiashara

Kundi la wanamgambo wa Kiislam la Al Shabab limedai kuhusika na shambulio hilo, lililotokea Alhamisi wiki hii.

Mlipuko huo, mojawapo ya milipuko mikubwa iliyoikumba Mogadishu hivi karibuni, umetokea kwenye mtaa wa Maka Mukaram, ambako kunapatikana hoteli nyingi, maduka na migahawa, Mkuu wa polisi amelimbia shirika la Habari la Reuters.

"Zaidi ya watu kumi wameuawa. Hoteli moja imeteketea kwa moto na majengo kadhaa yameharibiwa na mlipuko Watu 20 waliojeruhiwa wamepelekwa hospitalini. Tundhani kuwa bado kuna watu waliokwama chini ya vifuzi vya nyumba," amesema mkuu wa polisi Abdullahi Ali.

Kwa mujibu wa msemaji wa kundi la wanamgambo wa Kiislam la Al Shabab lenye mafungamano na Al Qaeda, wapiganaji bado wako ndani ya hoteli iliyoshambuliwa, madai ambayo yamekanushwa na mkuu wa polisi.

Hata hivyo mapema leo asubuhi polisi imebaini kwamba kumetokea urushianaji risasi kati ya wanamgambo hao na polisi katika jengo moja lililo jirani ya hoteli iliyoshambulia.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.