Pata taarifa kuu
SUDAN-MAANDAMANO-SIASA

Sudan yakumbwa na maandamano mapya

Sudan yaendelea kukumbwa na maandamano, Machi 18, 2019.
Sudan yaendelea kukumbwa na maandamano, Machi 18, 2019. © AFP

Wananchi wenye hasira nchini Sudan wamemiminika mitaani leo Jumatatu katika mji mkuu Khartoum, kwa mujibu wa mashahidi, ili kuendelea na maandamano yaliyoanzishwa Desemba 19 dhidi serikali ya rais Omar al-Bashir.

Matangazo ya kibiashara

"Uhuru, amani, haki," wameimba maelfu ya waandamanji ambao kwa kipindi cha miezi mitatu wanaomba rais Bashir kujiuzulu, wakimshtumu kutumia vibaya uchumi wa nchi.

Omar al-Bashir anatawala nchi ya Sudan kwa mkono wa chuma tangu alipoingia madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi mnamo mwaka 1989.

Leo Jumatatu, waandamanaji wameandamana katika eneo la Bahari, kaskazini mwa mji mkuu, na katika mtaa wa 60 mjini Khartoum, mashahidi wamesema. Polisi wametumia mabomu ya machozi dhidi ya waandamanaji waliokuwa wakiandamana katika mtaa wa 60, kwa mujibu wa vyanzo hivyo.

Wanafunzi pia wameandamana katika chuo kikuu cha mji wa Khartoum, kwa mujibu wa mashahidi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.