Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-AJALI-USALAMA

Ethiopian Airlines: Ripoti ya awali ya uchunguzi kutolewa wiki hii

Uchunguzi wa awali kuhusu ajali ya ndege ya Ethiopian Airlines unatarajiwa kutolewa kwa mujibu wa msemaji wa Wizara ya Usafiri ya Ethiopia.
Uchunguzi wa awali kuhusu ajali ya ndege ya Ethiopian Airlines unatarajiwa kutolewa kwa mujibu wa msemaji wa Wizara ya Usafiri ya Ethiopia. REUTERS/Baz Ratner

Ripoti ya awali ya uchunguzi kuhusu ajali ya ndege aina ya Boeing 737 MaX 8 ya shirika la ndege la Ethiopia, Ethiopian Airlines, ambayo iliua watu 157 Machi 10 "kuna uwezekano mkubwa" itolewe wiki hii, msemaji wa Wizara ya Usafiri ya Ethiopia amesema.

Matangazo ya kibiashara

"Inawezekana kutolewa wiki hii lakini mambo yasiyotabiriwa yanaweza kutokea," Muse Yiheyis ameliambia shirika la Habari la Reuters. "Siwezi kusema (kama itatolewa) leo au kesho," ameongeza.

Ndege karibu zote za ain aya Boeing 737 MAX 8 na 9 zimepigwa marufuku kusafiri tangu kutokea kwa ajali ya ndege ya Ethiopia, ambayo ilitanguliwa na ajali nyingine ya ndege kama hiyo ya Boeing 737 MAX ya shirika la ndege la Lion Air la Indonesia mwezi Oktoba na kuua watu 189.

Uchunguzi wa awali kuhusu data ya ndege hiyo inaonyesha "mazingira ya kufanana" kati ya ajali hizo mbili, wamesema wachunguzi wa Ethiopia na wenzao wa Ufaransa kutoka Ofisi ya Upelelezi na Uchambuzi (BEA).

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.