Pata taarifa kuu
ALGERIA-MAANDAMANO-SIASA-UCHAGUZI

Jeshi lachangia kujiuzulu kwa Bouteflika

Wanachi wa Algeria washerehekea hatua ya rais Bouteflika kujiuzulu, Algiers tarehe 2 Aprili 2019.
Wanachi wa Algeria washerehekea hatua ya rais Bouteflika kujiuzulu, Algiers tarehe 2 Aprili 2019. © REUTERS/Ramzi Boudina

Nchi ya Algeria imefungua ukurasa wa utawala wa rais Abdelaziz Bouteflika baada ya kuhudumu kwa takriban miaka 20, hatimaye ameondoka madarakani baada ya kutangaza kujiuzulu kufuatia shinikizo kutoka kwa wananchi walioandamana sasa ni zaidi ya majuma 6 huku yakiungwa mkono na jeshi.

Matangazo ya kibiashara

Vifijo na nderemo vimetawala Jumanne usiku katika miji mbalimbali nchini Algeria baada ya hatua hiyo ya kujiuzulu kwa rais Bouteflika ambae amekabidhi barua yake ya kujiuzulu kwa Mwenyekiti wa Baraza la kikatiba.

Raia wengi wa Algeria wanaamini kwamba hii ni hatua ya kwanza ya ushindi na wataendelea na maandamano kuhakikisha jopo zima la Bouteflika linaondoka.

Jeshi nchini humo limechangia pakubwa kuhakikisha Rais Bouteflika anaondoka haraka iwezekanavyo baada ya kuahidi kuwa atajiuzulu kabla ya April 28.

Jeshi la Algeria ambalo lina nguvu, lilimtaka kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 82 kutangaza kuwa hana uwezo wa kutekeleza majukumu yake ya uongozi.

Abdelaziz Bouteflika alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Kiharusi, miaka sita iliyopita na tangu hapo mara chache amekuwa akionekana katika sehemu za umma.

Machi 26 na Machi 30, Mkuu wa jeshi la Algeria alisema kuwa suluhisho la mgogoro linapatikana katika utekelezaji wa Ibara ya 102 ya Katiba, katika mchakato wa rais kutowajibika ten akwa mamlaka yake.

Tangu wakati huo rais Bouteflika alianza kupoteza imani kwa vigogo kutoka chama chake na washirika wake.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.