Pata taarifa kuu
ALGERIA-MAANDAMANO-SIASA-UCHAGUZI

Wananchi wa Algeria washerehekea kuondoka kwa Bouteflika, shinikizo laendelea

Walgeria wanasherehekea mitaani jijini Algiers hatua ya kujiuzulu kwa rais Abdelaziz Bouteflika, Aprili 2, 2019.
Walgeria wanasherehekea mitaani jijini Algiers hatua ya kujiuzulu kwa rais Abdelaziz Bouteflika, Aprili 2, 2019. © REUTERS/Ramzi Boudina

Tangazo la kujiuzulu kwa rais Abdelaziz Bouteflika limefuatiwa na matukio ya furaha jijini Algiers na miji mingine. Lakini wawanchi karibu wote wanasisitiza kuwa kuondoka kwa rais Bouteflika ni mwanzo tu.

Matangazo ya kibiashara

Jumanne usiku, wakati tangazo lilipotoplewa, makundi ya vijana waliingia mitaani wakielekea katikati mwa mji, huku wakiomba.

Vifijo na nderemo vimetawala Jumanne usiku katika miji mbalimbali nchini Algeria baada ya hatuwa hiyo ya kujiuzulu kwa rais Bouteflika ambae amekabidhi barua yake ya kujiuzulu kwa Mwenyekiti wa Baraza la kikatiba.

Raia wengi wa Algeria wanaamini kwamba hii ni hatuwa ya kwanza ya ushindi na wataendelea na maandamano kuhakikisha jopo zima la Bouteflika linaondoka.

Hatua ya kujiuzulu kwa rais Abdelazizi Bouteflika imekuja baada ya jeshi kutoa msimammo wake na kuomba Mahakam ya Katiba kutekeleza Ibara ya 102 ya Katiba inayozungumzia mchakato wa rais asiyewajibika kwa mamlaka yake.

Msimamo huo wa jeshi ulikuja kuunga mkono maandamano ya wananchi ambayo yalianza tangu wiki kadhaa zilizopita.

Waandamanaji wamekuwa wakiomba rais Bouteflika afute hatua yake ya kuwania kwa muhula wa tano katika uchaguzi ujao, jambo ambalo Bouteflika alifanya, lakini maandamano yaliendelea na kumtaka ajiuzulu.

Hata hivyo jeshi limechangia pakubwa kuhakikisha rais Bouteflika anaondoka haraka iwezekanavyo baada ya kuahidi kuwa atajiuzulu kabla ya April 28.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.