Pata taarifa kuu
LIBYA-MAPIGANO-USALAMA

Mapigano yarindima karibu na Tripoli, Libya

Marshal Khalifa Haftar, kiongozi wa kundi la wapiganaji wanaodhibiti mashariki mwa Libya.
Marshal Khalifa Haftar, kiongozi wa kundi la wapiganaji wanaodhibiti mashariki mwa Libya. REUTERS/Philippe Wojazer

Majeshi ya Marshal Haftar yanaendelea kusonga mbele Magharibi mwa Libya, na yamekabiliana na wapiganaji wenye silaha wa Waziri Mkuu anaye tambuliwa na jumuiya ya kimataifa Fayez al Serraj, kusini mwa Tripoli, kwa mujibu wa shrika la Habari la Reuters likimnukuu msemaji wa kundi hilo na wakaazi wa eneo hilo.

Matangazo ya kibiashara

Tangu kuanguka kwa utawala wa Muammar Gaddafi mnamo mwaka 2011, Libya imegawanywa mara mbili: Serikali ya umoja wa kitaifa (GNA) yenye makao yake makuu jijini Tripoli, inayotambuliwa kimataifa, na serikali nyingine, inayoungwa mkono na Marshal Khalifa Haftar, inadhibiti mashariki mwa nchi.

Baada ya kupanua udhibiti wake hivi karibuni kusini mwa Libya, jeshi linaloongozwa na Marshal Haftar (ANL) linaendelea kusonga mbele Magharibi mwa nchi, kama zinavyoonyesha picha zilizorushwa Jumatano wiki hii na vyombo vya habari rasmi vya ANL.

Makabiliano makali yaliyodumu saa moja yalitokea Jumatano usiku wiki hii karibu na jiji la Gharyan, mji wa kusini mwa Tripoli, kati ya wapiganaji wa ANL na vikosi vinavyomuunga mkono Waziri Mkuu Fayez al Serraj, msemaji wa ANL, Ahmed Mismari, amesema kwenye televisheni ya Al Arabiya.

Hakuna ushahidi wowote unaothibitisha ikiwa kuna watu waliouawa au kujeruhiwa.

Serikali inayo tambuliwa na jumuiya ya kimataifa haijatoa maelezo yoyote kuhusiana na mapigano hayo.

Makabiliano kati ya pande hizo mbili ni pigo kubwa kwa Umoja wa Mataifa na nchi za Magharibi ambao wanajaribu kupatanisha pande hizi, na wakati ambapo Serraj na Haftar walikutana mwezi uliopita huko Abu Dhabi kwa mazungumzo.

Mnamo mwezi Mei 2018 jijini Paris, wadau wakuu katika mgogoro wa kisiasa nchini Libya walikubaliana kuhusu kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu mnamo Desemba 10, lakini mwezi Novemba mwaka jana, mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Libya, Ghassan Salamé, alitangaza kuwa Umoja wa Mataifa umeachana na kalenda hiyo kwa sababu ya machafuko na mvutano wa kisiasa kati ya pande mbili hasimu.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.