Pata taarifa kuu
ALGERIA-MAANDAMANO-SIASA-UCHAGUZI

Algeria kukumbwa na maandamano makubwa baada ya kujiuzulu kwa Bouteflika

Maandamano ya leo Ijumaa yatakuwa ya kwanza tangu Abdelaziz Bouteflika ajiuzulu kwenye wadhifa wake, ni maandamano ya saba tangu kuanza kwa maandamano hayo (picha ya kumbukumbu).
Maandamano ya leo Ijumaa yatakuwa ya kwanza tangu Abdelaziz Bouteflika ajiuzulu kwenye wadhifa wake, ni maandamano ya saba tangu kuanza kwa maandamano hayo (picha ya kumbukumbu). REUTERS/Ramzi Boudina

Maelfu ya watu wanatarajia kuingia mitaani leo Ijumaa hii, Aprili 5 siku chache baada ya kujiuzulu kwa rais Abdelaziz Bouteflika, Maandamano hayo ni ni kwanza tangu kujiuzulu kwa rais Abdelaziz Bouteflika Jumanne jioni.

Matangazo ya kibiashara

Maandamano haya ni kipimo joto kwa mamlaka nchini Algeria.

 

Wiki hii kumekuwa na mabadiliko na ishara mbalimbali za matumaini nchini Algeria.

Mkuu wa majeshi, Ahmed Gaïd Salah, alisema kuwa suluhisho la katiba linapaswa kupendekezwa kupatia ufumbuzi maandamano hayo aambayo yanaendelea nchini Algeria.

Tayari wafanyabiashara, washirika wa karibu wa rais Abdelaziz Bouteflika, na wengi wao sasa wako chini ya uchunguzi wa awali kwa rushwa. Hatua ambayo ni muhimu, kwa vile majina ya wafanyabiashara hawa pia yalikuwa yakitajwa katika maandamano.

Tayari mfanyabiashara tajiri, anayeshtumiwa kuongoza katika rushwa kwa utawala wa Bouteflika, Ali Haddad, yuko gerezani.

Baadhi wanaamini kwamba jeshi liko upande wa raia na kwamba lazima walishukuru na kulipongeza kwa kazi nzuri linalofanya. Wengine wanaamini kuwa kuheshimu Katiba ni kisingizio tu, wakati Katiba ilirekebishwa kwa zaidi ya miaka 20 iliyopita, na wana wasiwasi kuhusu jukumu la kijeshi katika utawala mpya.

Kwa upande waangalizi wanasema, ikiwa jeshi liliomba rais ajiuzulu, ni kutaka kulinda vema taasisizi zilizopo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.