Pata taarifa kuu
CHAD-BOKO HARAM-USALAMA

Chad: Askari saba wauawa katika shambulizi la Boko Haram

Maeneo yaliyo pembezoni mwa ziwa Chad yameendelea kulengwa na mashambulizi ya Boko Haram, kama kijiji hiki cha Ngouboua, mwezi Aprili mwaka 2015.
Maeneo yaliyo pembezoni mwa ziwa Chad yameendelea kulengwa na mashambulizi ya Boko Haram, kama kijiji hiki cha Ngouboua, mwezi Aprili mwaka 2015. AFP PHOTO / PHILIPPE DESMAZES

Jeshi la Chad limepoteza askari wake saba na wengine kumi na tano kujeruhiwa katika shambulio la kundi la Boko Haram lililotokea katika Jimbo la Ziwa Chad.

Matangazo ya kibiashara

Mapigano kati ya jeshi la Chad na wanamgambo wa Kiislamu yamekuwa yamesitishwa kwa wiki tatu katika eneo hilo, baada ya wapiganaji hao kuanzisha mapigano kwa miezi kadhaa sasa.

Kituo cha jeshi cha Bohama karibu na mji wa Kaïga Kindjiria kwenye pwani ya kaskazini mwa Ziwa Tchad kimeshambuliwa usiku wa manane Jumatatu wiki hii. Washambuliaji, ikiwa ni pamoja na wale wa kujitoa muhanga, waliua askari saba wa Chad na kujeruhi wengine kumi na tano.

Waasi wengi wauawa

Washambuliaji sitini na watatu wameuawa kwa mujibu wa uongozi wa jeshi la Chad ambalo limebaini kwamba operesheni ya kuwatokomeza inaendelea. Mkuu wa majeshi, Jenerali Taher Erda, amekwenda eneo la tukio kwa helikopta mapema Jumatatu hii asubuhi.

Shambulizi hili, ambalo linatokea baada ya wiki tatu za utulivu, limeua idadi ndogo ya askari ikilinganishwa na lile la Dangdala, mji wa Chad, unaopatikana karibu na Niger. Wakati wa shambulio hilo, askari 20 wa Chad waliuawa na vifaa vya kijeshi kuporwa, hali ambayo ilisababisha baadhi ya wakuu wa jeshi kufutwa kazi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.