Pata taarifa kuu
MISRI-SIASA

Abdel Fattah al-Sisi kusalia madarakani hadi 2030

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sissi, Cairo, le MAchi 2, 2017.
Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sissi, Cairo, le MAchi 2, 2017. AFP/KHALED DESOUKI

Wabunge nchini Misri wameifanyia marekebisho Katiba ya nchi hiyo, kumruhusu rais Abdel Fattah al-Sisi kuendelea kusalia madarakani hadi mwaka 2030. Lakini wapinzani wake wamekosoa uamuzi huo wa bunge na kusema kuwa Misri inaingia katika utawala wa kiimla.

Matangazo ya kibiashara

Mbali na mabadiliko hayo, wabunge wamempa rais Al Sisi mamlaka makubwa ya kudhibiti idara ya Mahakama lakini pia jeshi kuendelea kuwa na usemi mkubwa katika siasa za nchi hiyo ya Afrika ya Kaskazini.

Hata hivyo, mabadiliko hayo yanatarajiwa kupigiwa kura ya maoni na wananchi wa Misri, na tarehe ya zoezi hilo inatarajiwa kutangazwa leo Jumatano.

Rais Al Sisi, ambaye alichaguliwa mwaka 2018, muhula wake wa miaka sita ulitarajiwa kumalizika mwaka 2024, lakini iwapo mabadiliko hayo yataungwa mkono, anaweza kuchagulia tena kwa muhula mwingine wa miaka sita.

Al Sisi aliingia madarakani mwaka 2013, baada ya kuongoza mapinduzi ya kijeshi kumpindua rais aliyekuwa amechaguliwa wakati huo Mohamed Morsi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.