Pata taarifa kuu
ALGERIA-MAANDAMANO-SIASA-UCHAGUZI

Algeria: Maandamano yaendelea, watu waendelea kukamatwa

Maandamano ya Ijumaa ya tisa tangu kuanza kwa maandamano ya kuung;oa utawala wa Abdelaziz Bouteflika, Aprili 19, 2019 .
Maandamano ya Ijumaa ya tisa tangu kuanza kwa maandamano ya kuung;oa utawala wa Abdelaziz Bouteflika, Aprili 19, 2019 . REUTERS/Ramzi Boudina

Maandamano makubwa yanatarajiwa kufanyika leo Ijumaa katika miji mbalimbali nchini Algeria. Waandamanaji wameapa kuendelea kuandamana hadi pale mfumo mzima wa utawala wa Abdelaziz Boueflika utakuwa umeondoka.

Matangazo ya kibiashara

Wiki hii maafisa na wafanyabiashara kadhaa walikamatwa wakishtumiwa kuwa na ukaribu na utawala wa abdelaziz Bouteflika.

Waziri wa zamani wa Nishati ni miongoni mwa watu vigogo waliokamatwa na vikosi vya usalama kwa amri ya vyombo vya sheria vya Algeria. Wakati huo huo, katika ujumbe, Ahmed Gaid Salah, Mkuu wa majeshi amesema kuwa mahakama itashughulikia kesi za rushwa.

Hatua zote hizo za jeshi, bado hazijapunguza hasira ya waandamanaji. Kwanza, kwa sababu waandamanaji wengi hawaamini ukweli wa operesheni hii vikosi vya usalama na jeshi. Wengine wamebaini kwamba viongozi wa juu hawajakamatwa. Wengine wanaona kwamba ni vita vya ukoo, kwa sababu wanaolengwa ni ndugu wa familia ya Bouteflika.

Hata hivyo maandamano ya kumuunga mkono Issad Rebrab, mmiliki wa Cevital, yalifanyika Alhamisi wiki hii katika Jimbo la Kabylie.

Wengi wameshtumu Mkuu wa Majeshi Ahmed Gaid Salah kuwa na ushawishi kwa vyombo vya sheria nchini Algeria, wakibaini kwamba jeshi halipaswi kuwa na ushawishi wala shinikizo kwa vyombo vya sheria.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.