Pata taarifa kuu
ISIL-ADF NALU-DRC-WAASI-USALAMA

Islamic State yadai kutekeleza shambulizi mjini Beni Mashariki mwa DRC

Magaidi wa Islamic State
Magaidi wa Islamic State REUTERS/Emmanuel Braun

Kundi la Islamic State limedai kutekeleza shambulizi katika mji wa Beni Mashariki mwa DRC, na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 10 wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Kupitia ujumbe ulioandikwa kupitia ukurasa wa Telegram kwenye mtandao wa kijamii, kundi hilo limesema lililenga kambi ya jeshi mjini Beni na kuwauawa au kuwajeruhi watu 25.

Kundi la Islamic State limeendelea kushirikiana na kundi la ADF Nalu kutekeleza mashambulizi Mashariki mwa nchi hiyo hasa Wilayani Beni, eneo ambalo linakabiliwa na ugonjwa hatari wa Ebola.

Wiki hii, iliripotiwa kuwa  waasi waliaminiwa kuwa wa ADF walitekeleza shambulizi  katika kambi ya jeshi la Rwangoma, lakini wakalemewa na kutoroka.

Mkuu wa Wilaya ya Rwangoma Richard Paluku, akunukuliwa akisema katika makabiliano hayo, wanajeshi wawili wa FARDC, walipoteza maisha.

Tangu mwaka 2014, makundi ya waasi wamekuwa wakiwashambulia katika makaazi yao, suala ambalo limewakasirisha wakaazi wa mji huo wakitaka serikali kufanya juhudi za kuimarisha usalama.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.