Pata taarifa kuu
MALAWI-SIASA-MUTHARIKA-UPINZANI

Rais Mutharika asema upinzani unataka kumpindua kwa nguvu

Rais wa Malawi  Profesa Peter Mutharika
Rais wa Malawi Profesa Peter Mutharika The Maravi Post

Rais wa Malawi, Peter Mutharika ameutuhumu upinzani nchini humo ambao umekataa kutambua ushindi wake katika uchaguzi wa mwezi Mei kwa kutaka kuipindua serikali yake kwa nguvu.

Matangazo ya kibiashara

Rais Mutharika anadai kuwa Lazarus Chakwera kiongozi mkuu wa upinzani na wafuasi wake wanapanga njama kuipindua serikali yake, wakati huu watu wanaounga mkono upinzani wakidai kiongozi wao aliibiwa kura.

Katika hatua nyingine, Balozi wa Marekani nchini Malawi Virginia Palmer alilazimika kukimbiasiku ya Alhamisi kutoka katika makao makuu ya chama cha upinzani cha Malawi Congress Party jijini Lilongwe baada ya polisi kurusha mabomu ya kutoa machozi.

Balozi Palmer amesema alikuwa amekwenda kumuaga kiongozi wa upinzani kabla ya kurejea nchini Marekani kwa sababu muda wake wa kuhudumu nchini Malawi, unafika mwisho wakati alipokabiliana na hali hiyo.

Chakwera ambaye alishindwa na rais Mutharika kwa kura karibu 190,000 amesema hawezi kukubali na kumtambua mpinzani wake kama rais na ataendelea kushinikiza haki kutendeka.

Tayari amewasilisha kesi Mahakamani kupinga ushindi wa rais Mutharika.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.