Pata taarifa kuu
RWANDA-UGANDA

Rwanda yafungua kwa muda mpaka wake na Uganda

Rais wa Rwanda, Paul Kagame akiwa kwenye moja ya mahojiano na RFI
Rais wa Rwanda, Paul Kagame akiwa kwenye moja ya mahojiano na RFI RFI/F24

Baada ya kufungwa kwa karibu miezi mitatu, mamlaka nchini Rwanda zimeufungua kwa muda mpaka wa nchi yake na Uganda ili kuruhusu magari ya mizigo kuvuka mpaka.

Matangazo ya kibiashara

Mvutano wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili ulisababisha kufungwa kwa shughuli za mpakani, hatua ambayo imeathiri pakubwa biashara na maisha ya watu wanaoishi kwenye maeneo ya mpaka wa Gatuna.

Inakadiriwa kuwa asilimia 70 ya biashara za kwenye mpaka wa nchi hizo mbili zilisimama, mamlaka za Uganda zimesema.

Mwezi February, nchi ya Rwanda ilitangaza kufunga mpaka wake mkuu wa Gatuna, ikisema inaufanyia marekebisho na kukanusha kuwa ulikuwa ni uamuzi wa kisiasa.

Katika taarifa yake ya awali, Rwanda ilikataza raia wakew kuvuka mpaka kwenda Uganda kwa kile ilisema ni sababu za kiusalama.

Hivi sasa mamlaka ya mapato nchini Rwanda inasema mpaka huo umefunguliwa kwa muda kutathmini namna ambavyo maboresho waliyoyafanya yanafanya kazi.

Nchi ya Rwanda inaituhumu Uganda kwa kuwakamata kinyume cha sheria raia wake pamoja na kuwatesa.

Kwa upande wake nchi ya Uganda inaituhumu Rwanda kwa kufanya ujasusi nchini mwake.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.