Pata taarifa kuu
CHAD-WAAS-UFARANSA-SIASA-SUDAN

Kiongozi wa waasi nchini Chad azuiwa nchini Ufaransa

Kiongozi  wa waasi Jenerali Mahamat Nouri
Kiongozi wa waasi Jenerali Mahamat Nouri www.francebleu.fr

Mmoja wa viongozi wa waasi nchini Chad Jenerali Mahamat Nouri, amezuiwa jijini Paris nchini Ufaransa kwa madai ya uhalifu wa kivita, uliotokea nchini Sudan.

Matangazo ya kibiashara

Jenerali Nouri, anayeongoza kundi la waasi wa UFDD amekuwa akizuiwa nyumbani kwake Magharibi mwa jiji la Paris.

Anatuhumiwa kuongoza vikosi vyake kutekeleza mauaji nchini Sudan kati ya mwaka 2005-2010.

Viongozi wa mashtaka nchini Ufaransa wanasema pamoja na Jenerali Nouri, wamewakamata pia waasi wawili, wakati huu wakiendelea na uchunguzi zaidi.

Kundi la UFDD limekuwa pinzani kwa uongozi wa serikali ya rais Idriss Deby Itno na mwaka 2008 walijaribu kumpindua raus huyo lakini wakalemewa na wanajeshi wa serikali karibu na Ikulu jijini N'Djamena.

Kabla ya kukimbilia nchini Ufaransa, Jenerali Nouri alikuwa anaishi Qatar.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.