Pata taarifa kuu
DRC-WHO-AFYA

Shirika la Afya Duniani WHO lafunga milango Beni

Maafisa wa afya wa DRC na wale wa Shirika la Afya Duniani wakivalia mavazi ya kujikinga dhidi ya Ebola wakati walipokuwa wakishiriki katika mafunzo ya kupambana dhidi ya Ebola karibu na mji wa Beni Agosti 11, 2018.
Maafisa wa afya wa DRC na wale wa Shirika la Afya Duniani wakivalia mavazi ya kujikinga dhidi ya Ebola wakati walipokuwa wakishiriki katika mafunzo ya kupambana dhidi ya Ebola karibu na mji wa Beni Agosti 11, 2018. REUTERS/Samuel Mambo

Shirika la afya duniani WHO, limetangaza kusitisha shughuli zote za kutoa huduma za afya katika eneo la Beni, lililoathiriwa na ugojwa hatari wa Ebola.

Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa operesheni za dharura za WHO barani Afrika na katika eneo la Ituru na Kivu Kaskazini, Daktari Michel Yao, ametangaza hatua hiyo baada ya vijana wenye hasira kuteketeza moto gari lao katika Manispaa ya Mulekera.

Hali hiyo imeleta wasiwasi mkubwa katika maeneo ya Beni, huku maafisa wa faya wakuhofia usalama wao.

Aidha, Daktari huyo amesema kuwa katika mazingira hayo, ni vigumu kuendelea kufanya kazi kwa sababu wahudumu wa afya wanahofia maisha yao.

Hatua hii inakuja, baada ya ripoti kuwa watu 1,500 wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa huo tangu mwezi Agosti mwaka uliopita, Mashariki mwa nchi hiyo.

Watu wengine zaidi ya elfu mbili, wameambukizwa na laki moja na elfu aroboini kupewa chanjo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.