Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-MACHAFUKO-USALAMA-HAKI

Jaribio la mapinduzi Ethiopia: Sita wafikishwa mahakamani kwa ugaidi

Mji wa Lalibela katika Jimbo la Amhara, Ethiopia. (Picha ya kumbukumbu)
Mji wa Lalibela katika Jimbo la Amhara, Ethiopia. (Picha ya kumbukumbu) REUTERS/Thomas Mukoya

Watu 6 wamefikishwa mahakamani kwenye mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa na kushtakiwa kwa makosa ya ugaidi kuhusiana na jaribio la mapinduzi ya Serikali ya Jimbo la Amhara.

Matangazo ya kibiashara

Wanakuwa watu wa kwanza kufikishwa mahakamani tangu kushuhudia kwa machafuko ya siku ya Jumamosi iliyopita, ambapo mnadhimu mkuu wa jeshi Jenerali Seare Mekonnen na watu wengine wanne waliuawa.

Katika vurugu za mwishoni mwa juma lililopita, kinara anayetuhumiwa kuandaa jaribio hilo Brigedia Jenerali Asaminew Tsige nae aliuawa na vyombo vya usalama.

Mkuu wa Jeshi la Ethiopia Jenerali Seare Monnen, aliuawa kwa kupigwa risasi na mlinzi wake mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Jenerali Seare Mekonnen na maafisa wengine watatu wa ngazi za juu waliuawa katika jaribio la kuipindua serikali ya jimbo la Amhara kaskazini mwa nchi hiyo.

Yeye na ofisa mwingine walipoteza maisha katika mji wa Amhara wakijaribu kuzuia mapinduzi dhidi ya utawala nchini humo, Waziri mkuu Abiy Ahmed alisema.

Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yameikumba Amhara na miji mingine miaka ya hivi karibuni.

Tangu uchaguzi wa mwaka jana,Abiy amekua akipambana kumaliza mvutano wa kisiasa kwa kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa, kuondoa makatazo dhidi ya vyama vya kisiasa na kuwashtaki maafisa wanaoshutumiwa kukiuka haki za binaadamu.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.