Pata taarifa kuu
TUNISIA-USALAMA

Tunisia: Polisi mmoja auawa, watu kadhaa wajeruhiwa katika milipuko miwili Tunis

Polisi nchini Tunisia imelengwa na mashambulizi mawili ya mabomu yaliotekelezwa na watu wa kujitoa muhanga.
Polisi nchini Tunisia imelengwa na mashambulizi mawili ya mabomu yaliotekelezwa na watu wa kujitoa muhanga. FETHI BELAID/AFP

Milipuko miwili ya mabomu imesikika katika mji mkuu wa Tunisa, Tunis, na kusababisha watu wengi kujeruhiwa, kwa mujibu wa vyanzo vya polisi.

Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi hayo yamelenga polisi, kulingana na duru za kuaminika. Kwa sasa, inaarifiwa kuwa afisa mmoja wa polisi amepoteza maisha.

Shambulizi la kwanza la kujitoa muhanga lilitokea kwenye mtaa mkuu wa mji wa Tunis, kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, ikinukuliwa na shirika la Habari la AFP.

Raia watatu na polisi wawili wamejeruhiwa. Viungo vya miili vimetapakaa barabarani karibu na gari la polisi kwenye mtaa wa Bourguiba, karibu na ubalozi wa Ufaransa na mji wa kale, mwandishi wa habari wa AFP amebaini.

"Hili ni shambulio la kujitoa muhanga, lililotokea saa 10:50," amesema msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Sofiene Zaag, akiliambia shirika la Habari la AFP. Kikosi cha usalama wa raia na polisi wametumwa katika mtaa wa Bourguiba, kunakopatikana makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani.

Muda mfupi baada ya hapo, mshambuliaji mwengine wa kujitoa muhanga alijilipua karibu na kituo cha polisi katika wilaya ya Al Karjani, jijini Tunis, na kusababisha watu wanne kujeruhiwa, Wizara ya mambo ya Ndani imeongeza.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.