Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-MACHAFUKO-USALAMA

Watu zaidi ya 200 wakamatwa Ethiopia kufuatia jaribio la mapinduzi

Waziri mkuu Abiy Ahmed, mwenye umri wa miaka 42, amepata sifa za kimataifa ushirikiano wa kikanda na kuboresha maridhiani nchini Ethiopia.
Waziri mkuu Abiy Ahmed, mwenye umri wa miaka 42, amepata sifa za kimataifa ushirikiano wa kikanda na kuboresha maridhiani nchini Ethiopia. REUTERS/Tiksa Negeri/File Photo

Vyombo vya usalama nchini Ethiopia vimewakamata watu zaidi ya 200 wakiwemo raia wa kawaida, wanausalama na wanasiasa wanaotuhumiwa kuhusika katika jaribio la mapinduzi kwenye Jimbo la Amhara, ambako rais wa eneo hilo na mnadhimu wa jeshi waliuawa.

Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi ya mwishoni mwa juma lililopita, yamezidisha shinikizo zaidi kwa utawala wa waziri mkuu Abiy Ahmed ambaye ameendelea kukabiliana na changamoto za machafuko ya kikabila na mabadiliko ya uchumi wa taifa hilo.

Machafuko hayo, ambayo serikali inasema yalikuwa sehemu ya njama iliyofanywa na Jenerali mmoja muasi na wanajeshi wake kuchukua udhibiti wa Amhara, yalidhihirisha namna mivutano ya kikabila inavyotishia ajenda ya mageuzi ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed.

Waziri mkuu Abiy Ahmed, mwenye umri wa miaka 42, amepata sifa za kimataifa ushirikiano wa kikanda na kuboresha maridhiani nchini Ethiopia, lakini wachambuzi wanasema mabadiliko ya kasi yamezusha hali ya sintofahamu na ukosefu wa usalama.

Tayari watu 6 wamefikishwa mahakamani kwenye mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa na kushtakiwa kwa makosa ya ugaidi kuhusiana na jaribio la mapinduzi ya Serikali ya Jimbo la Amhara.

Katika vurugu za mwishoni mwa juma lililopita, kinara anayetuhumiwa kuandaa jaribio hilo Brigedia Jenerali Asaminew Tsige nae aliuawa na vyombo vya usalama.

Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yameikumba Amhara na miji mingine miaka ya hivi karibuni.

Tangu uchaguzi wa mwaka jana,Abiy amekua akipambana kumaliza mvutano wa kisiasa kwa kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa, kuondoa makatazo dhidi ya vyama vya kisiasa na kuwashtaki maafisa wanaoshutumiwa kukiuka haki za binaadamu.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.