Pata taarifa kuu
DRC-SIASA

Serikali mpya ya DRC kutangazwa kabla ya Agosti 15

Rais Felix Tshisekedi (kulia) Na Waziri Mkuu mpya Sylvester Ilunga Ilunkamba.
Rais Felix Tshisekedi (kulia) Na Waziri Mkuu mpya Sylvester Ilunga Ilunkamba. © Présidence de la République démocratique du Congo

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Sylvestre Ilunga Ilunkamba ameanza mazungumzo ya kuunda serikali, karibu wiki 11 baada ya kuteuliwa katika nafasi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Wananchi wa taifa hilo wamekuwa wakisubiri Mawaziri wapya, baada ya kuingia madarakani kwa rais Felix Tshisekedi baada ya Uchaguzi Mkuu wa Desemba 30 mwaka 2018.

Mazungumzo haya yamekuja, baada ya makubaliano kati ya muungano wa kisiasa wa rais wa zamani FCC Joseph Kabila na CACH ule wa rais Felix Tshisekedi kuunda serikali ya muungano ya Mawaziri 65.

Rais Felix Tshisekedi na Waziri wake Mkuu tayari wameshauriana na kupokea watu mbalimbali, tangu kumalizika kwa mazungumzo kuhusu kugawana nyadhifa kati ya FCC na CACH.

Serikali mpya inatarajiwa kutangazwa siku chache zijazo, kabla ya Agosti 15 mwaka huu, chanzo kilio karibu na rais kimesema.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.