Pata taarifa kuu
UGANDA-ZAMBIA-HUAWEI-SIASA

Huawei yaombwa kupeleleza upinzani nchini Uganda na Zambia

Kulingana na Gazeti la Wall Street Journal, Huawei ilitoa taarifa za kibinafsi za wapinzani wa kisiasa kwa serikali za Uganda na Zambia.
Kulingana na Gazeti la Wall Street Journal, Huawei ilitoa taarifa za kibinafsi za wapinzani wa kisiasa kwa serikali za Uganda na Zambia. © FRED DUFOUR / AFP

Kampuni ya simu ya Huawei inaendelea kukumbwa na upinzani mkubwa wa kibiashara, lakini kwa sasa barani Afrika. Gazeti la Wall Street Journal lilichapisha Jumatano (Agosti 14) uchunguzi kuhusu uhusiano kati ya serikali za Kiafrika na wafanyakazi wa kampuni hiyo ya China katika nchi hizo za Afrika.

Matangazo ya kibiashara

Gazeti hilo la Marekani, limezinyooshea kidole serikali za Uganda na Zambia. Mamlaka katika nchi zote hizo mbili wameomba msaada ili kupata habari za kibinafsi kutoka kwa wanasiasa wengine. Lengo ikiwa ni kutaka serikali zilizopo ziendelea kusalia madarakani, na kuangamiza kabisa upinzani.

Wafanyakazi wa shirika hilo la simu la Huawei wameanza kufanya udukuzi wa mawasiliano ya simu za wanasiasa wa upinzani wa nchi hizo mbili kupitia Pegasus, mfumo wa upelelezi kutoka Israeli. Mfumo huo unaruhusu kupata ujumbe, kutumia microphone, au kamera ya simu inayofanyiwa udukuzi.

Nchini Uganda, hali hiyo ilianza mwaka 2018. Mamlaka mjini Kampala ilitumia mafundi kufanya udukuzi kwenye akaunti za WhatsApp na Skype za mwanamuziki maarufu na mbung Bobi Wine. Mwanamuziki huyo, ambaye ni mbunge tangu mwezi Juni 2017, ni mkosoaji mkubwa wa Rais Yoweri Kaguta Museveni. Lengo ilikuwa kumzuia na kumshusha kiongozi huyo wa upinzani ambaye ni maarufu nchini Uganda.

Bila maelezo zaidi, Serikali ya Uganda imethibitisha kuwa ina uhusiano na kampuni ya simu ya Huawei. Serikali ya Uganda imeeleza kwamba mafundi wa Huawei wanafanya kazi na polisi na maafisa wa idara ya ujasusi kwa malengo ya usalama wa taifa.

Nchini Zambia, wafanyakazi wa kampuni hiyo ya China walisaidia kufuatilia wanablogu muhimu ambao ni wakosoaji wakuu wa Rais Edgar Lungu. Wafanya udukuzi wa simu na kurasa za Facebook ili waweze kujuwa waliko, halafu wakamatwe.

Hapa pia, mamlaka nchini Zambia imejibu Gazeti la Wall Street Journal na kukubali kufanya kazi kwa ushirikiano na kampuni ya simu kutoka China ya Huawei, lakini sio kwa madhumuni ya kufanya udukuzi, bali kuwakamata waandishi wa "Habari bandia".

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.