Pata taarifa kuu
SUDANI-SIASA-USALAMA

Sudan: Abdalla Hamdok, ateuliwa kwenye nafasi ya waziri mkuu

Waziri Mkuu mpya wa Sudani Abdallah Hamdok aliapishwa Jumatano, Agosti 21, 2019 Khartoum.
Waziri Mkuu mpya wa Sudani Abdallah Hamdok aliapishwa Jumatano, Agosti 21, 2019 Khartoum. © Ebrahim HAMID / AFP

Hatimaye Waziri Mkuu mpya wa Sudani Abdallah Hamdok, 61, amekula kiapo mbele ya rais wa Baraza Kuu Tawala. Bw Hamdok atakuwa na kibarua cha kuimarisha hali ya uchumi ambao umeendelea kudorora.

Matangazo ya kibiashara

Abdalla Hamdok, ambaye alizaliwa wakati Sudani ilikuwa katika mchakato wa kupata uhuru mnamo mwaka 1956 katika eneo la Kordofan Kusini, alianza masomo yake ya chuo kikuu katika kitivo cha uchumi jijini Khartoum mnamo miaka ya 1970. Wakati huo, ilikuepo redio moja tu ya Omdurman ambayo ilikuwa ikitangaza majina ya wanafunzi waliokubaliwa katika chuo kikuu. Hapo ndipo alipoanza shughuli zake za kisiasa. Hata hivyo aliamua kuendelea na masomo yake.

Hamdok anakuwa mtu wa kwanza kushika madaraka ya kiraia tangu Omar el-Bashir alipoingia madarakani mnamo 1993. Abdalla Hamdok anatarajiwa kuteua serikali na kuongoza nchi kwa miezi 39.

Serikali hii mpya inayotarajiwa itakuwa na kazi ngumu kwa kurejesha usalama, kudumisha umoja na kuweka sawa uchumi ambao umeendelea kudorora.

Kipindi cha mpito kuelekea utawala wa kiraia nchini Sudan, kufuatia mkataba wa kihistoria kati ya jeshi na viongozi wa maandamano, kilianza Jumatano hii, Agosti 21 na kwa kutawazwa kwa rais wa Baraza Kuu Tawala.

Rais mpya wa Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, aliapishwa mbele ya mamlaka ya juu zaidi nchini humo. Wajumbe wengine kumi wa Baraza Kuu Tawala walikula kiapo mbele ya rais. Uteuzi rasmi wa waziri mkuu unatarajiwa leo kufanyika baadaye leo jioni.

Chini ya masharti ya mkataba wa kisiasa uliyotiwa saini Jumamosi, Agosti 17, Abdel Fattah al-Burhan ataongoza Sudan kwa kipindi cha miezi ishirini na moja, kabla ya kukabidhi madaraka kwa raia ambaye ataongoza nchi hiyo kwa kipindi cha miezi kumi na nane kitakacho salia.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.