Pata taarifa kuu
NIGERIA-AFRIKA KUSINI-USALAMA

Raia wa Nigeria zaidi ya 600 waanza kuondoshwa Afrika Kusini

Watu zaidi ya 12 waliuawa katika ghasia zinazotokana na chuki Afrika Kusini.
Watu zaidi ya 12 waliuawa katika ghasia zinazotokana na chuki Afrika Kusini. AFP/Michel Spatari

Nigeria imeanza zoezi la kuwaondoa raia wake waishio nchini Afrika Kusini, ambao wameoredheshwa kwenye ubalozi wa nchi hiyo nchini Afrika Kusini. Watu 640 ndio wanatarajiwa kusafirishwa kutoka Johannesburg kwenga Nigeria.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nchi za nje ya Nigeria kwenye ukurasa wake wa twitter inakadiriwa kuwa idadi ya raia 313 watachukuliwa kutoka Afrika Kusini katika awamu ya kwanza na waliosalia watasafirishwa siku za Alhamisi na Ijumaa wiki hii.

Serikali ya Nigeria tayari iliwaonya raia wake waliopo Afrika Kusini wasisafiri ama kuelekea kwenye maeneo ambayo ghasia hizo zimeshamiri mpaka pale hali itakapotengemaa.

Wizara ya mambo ya Nje ya Nigeria ilisema mmliliki wa Shirika la Ndege la Air Peace yupo tayari kuwasafirisha bure wale wote watakaotaka siku ya Ijumaa.

Awali waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria Geoffrey Onyeama aliwaambia wanahabari siku ya Jumatano wiki iliyopita kuwa kulingana na taarifa zilizowafikia, hakuna raia wa Nigeria aliyepoteza uhai kwenye ghasia zinazoendelea.

Rais Muhammadu Buhari alisema kuwa anamtuma mwakilishi wake kwenda Afrika Kusini kueleza 'ghadhabu' zao juu vurugu zinazoendelea.

Hatua hiyo inakuja wakati uhusiano kati ya nchi hizo mbili umeanza kuwa mzuri, baada ya kukumbwa hali ya sintofahamu kwa wiki moja iliyopita . Baada ya mvutano wa siku kadhaa, Abuja ilimtuma mjumbe wake kwenda Afrika Kusini na ikasema kwamba inataka kutafuta suluhisho na Pretoria. Na wakuu wa nchi hizi mbili wanatarajia kukutana mapema mwezi Oktoba nchini Afrika Kusini.

Mvutano kati ya nchi hizi mbili zenye nguvu kiuchumi barani Afrika unaweza kusababisha athari kubwa. Wiki iliyopita, Nigeria ilisusia Mkutano wa Uchumi wa Dunia uliofanyika jijini Cap, nchini Afrika Kusini.

Mtu mwengine aliuawa Johannesburg, mwishoni mwa wiki hii iliyopita na kufikia 12 idadi ya watu kutoka nchi za kigeni ambao wameuawa katika ghasia zinazochochewa na chuki dhidi ya wageni zilizozuka tangu wiki iliyopita nchini humo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.