Pata taarifa kuu
DRC-AJALI-USALAMA

Ajali mbaya ya treni yaua watu zaidi ya 50 Tanganyika, DRC

Treni iliyojaa mzigo inaondoka Kinshasa, DRC.
Treni iliyojaa mzigo inaondoka Kinshasa, DRC. © Per-Anders Pettersson/Getty Images

Treni imeanguka mapema Alhamisi asubuhi katika mji wa Tanganyika, Kusini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kuua watu zaidi ya hamsini. Mpaka sasa, haijajulikana idadi rasmi ya watu ambao wamefariki dunia katika ajali hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Awali Waziri wa Mambo ya Kibinadamu alisema watu zaidi ya 50 walifariki katika ajali hiyo.

Kulingana na manusura, ajali hiyo ilitokea karibu saa tatu asubuhi katika mji wa Mayibaridi, katika mkoa wa Tanganyika kusini mashariki mwa DRC.

Treni ilikuwa inatumikia maeneo ya Nyunzu na Nyemba.Treni hiyo ilipoteza muelekeo, Kuanguka kwa bewa mbili ndipo kumesababisha ajali hiyo.

Abiria kadhaa wamefariki dunia, waathiriwa wengine huenda wangekuwa chini ya magari ya bidhaa.

Waziri wa Mambo ya Kibinadamu wa DRC, Steve Mbikayi, amesema watu 50 wamepoteza maisha na 23 wamejeruhiwa. Uongozi wa shirika la reli nchini Zimbabwe, SNCC, umethibitisha kwamba watu wengi wamejeruhiwa, bila hata hivyo kutoa idadi rasmi ya watu waliojeruhiwa.

Upande wa serikali ya mkoa wa Tanganyika, Dieudonne Yumba, Waziri wa Mambo ya ndani na msemaji, amesema anajizuia kuzungumza chochote kabla hajapata ripoti ya maafisa waliotumwa katika eneo la tukio.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.