Pata taarifa kuu
TUNISIA-UCHAGUZI-SIASA

Raia wa Tunisia wasubiri kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais

Watu waliojitolea wakishiriki zoezi la uhesabuji kura katika ofisi moja jijini Sousse Septemba 15, 2019.
Watu waliojitolea wakishiriki zoezi la uhesabuji kura katika ofisi moja jijini Sousse Septemba 15, 2019. © ANIS MILI / AFP

Wananchi wa Tunisia, wanasubri matokeo ya mshindi wa uchaguzi wa urais baada ya kupiga kura mwishoni mwa wiki iliyopita. Kiwango cha ushiriki kimefikia 45%.

Matangazo ya kibiashara

Karibu nusu ya wapiga kura walijitokeza kushiriki katika uchaguzi huo wa pili tangu kuondolewa madarakani kwa rais wa zamani Ben Ali kufutatia maandamano ya wananchi mwaka 2011.

Wagombea 26 wakiwemo wanawake wawili wanawania wadhifa huo. Matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutanagzwa Jumanne wiki hii.

Wagombea wawili katika uchaguzi huo wanadai kuwa wamepata kura unayowawezesha kuwania katika duru ya pili ya uchaguzi, lakini mpaka sasa pili hakuna takwimu rasmi.

Tangu Jumapili jioni, maafisa wa ISIE, mamlaka inayohusika na uchaguzi, wmeanza zoezi la kukusanya na kufanya uchaguzi wa matokeo ya uchaguzi kutoka mikoa 24 inayounda nchi hiyo.

Matokeo ya awali hayajatangazwa. Baadhi ya raia wa Tunisia waishio ugenini bado wanapiga kura kwenye balozi mbalimbali za nchi hiyo. Zoezi la kupiga kura kwa raia wa Tunisia linatarajiwa kukamilika Jumatatu hii asubuhi katika jimbo la San Francisco, nchini Marekani.

Lakini tayari, wagombea wawili watangaza kuwa wamepata kura zinazowawezesha kuwania katika duru ya pili ya uchaguzi kufuatia takwimu zilizotolewa Jumapili jioni na shirika moja lililofanya uchunguzi. Wagonea hao ni pamoja na mfanyabiashara Nabil Karoui, ambaye yuko kizuizini kwa kesi ya utakatishaji wa fedha, na Kais Saïed, ambaye ni mgombea binafsi.

Wakati huo huo mgombea wa Chama cha Kiisilamu cha Ennahdha Youssef Chahed amekiri kushindwa katika uchaguzi huo. Akihojiwa na vyombo vya habari nchini Tunisia, Youssef Chahed, amesema chama chake kimeshindwa kufanya vizuri katika uchaguzi huo, huku akisem ana masikitiko makubwa na huzuni kwa kuona hajafanya vizuri katika uchaguzi huo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.