Pata taarifa kuu
CAR-USALAMA

Watu 38 wauawa katika mapigano Jamhuri ya Afrika ya Kati

Sherehe ya kusaini makubaliano ya amani kati ya serikali ya Afrika ya Kati na makundi ya watu wenye silaha, Februari 6, 2019, Bangui.
Sherehe ya kusaini makubaliano ya amani kati ya serikali ya Afrika ya Kati na makundi ya watu wenye silaha, Februari 6, 2019, Bangui. https://twitter.com/UN_CAR

Mapigano kati ya makundi mawili nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati yanayomiliki silaha yamesabisha vifi vya watu 38. Watu wengi wamejeruhiwa katika mapigano hayo yaliyoyahusisha makundi mawili hasama ya kundi la Seleka.

Matangazo ya kibiashara

Hii ni katika hali ambayo makundi hayo, yalitia saini mkataba wa amani kwenye serikali ya umoja wa kitaifa nchini CAR.

Mapigano hayo yalianza mwishoni mwa wiki iliyopita, kwa mujibu a Tume ya Umoja wa Mataifa nchini humo MINUSCA.

Makabiliano haya yamejiri licha ya makundi yenye silaha kutia saini mkataba mwezi Februari, wakati huu Rais Faustin-Archange Touadera, akinukuliwa akisema mapema mwezi huu kuwa mkataba huo bado upo imara.

Umoja na Mataifa na Umoja wa Afrika wamelaani vikali kitendo cha kuibuka upya mapigano katika mji wa Birao wa kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati kwenye mpaka na Sudan Kusini.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.