Pata taarifa kuu
CARICC-HAKI

CAR: ICC yaanza kujadili mashtaka dhidi ya Ngaïssona na Yekatom

Kiongozi wa zamani wa kundi la wanamgambo wa Kikristo la Anti-balaka, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Patrice-Edouard Ngaïssona, mbele ya Mahakama ya Kimatiaf ya Uhalifu (ICC), Hague, Januari 2019.
Kiongozi wa zamani wa kundi la wanamgambo wa Kikristo la Anti-balaka, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Patrice-Edouard Ngaïssona, mbele ya Mahakama ya Kimatiaf ya Uhalifu (ICC), Hague, Januari 2019. © Koen van Weel / POOL / AFP

Kuanzia Alhamisi hii hadi 27 Septemba, majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) wanajadili mashtaka yaliyoletwa na mwendesha mashtaka dhidi ya viongozi wa zamani wa kundi la wanamgambo wa Kikristo anti-balaka Patrice-Edouard Ngaïssona na Alfred Yekatom.

Matangazo ya kibiashara

Patrice-Edouard Ngaïssona na Alfred Yekatom wanatuhumiwa uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita.

Wawili hao wanatuhumiwa mauaji, kuwatesa raia, visa vya watu kutoweka, ukatili, mashambulizi dhidi ya raia na mashambulizi dhidi ya misikiti. Orodha ni ndefu ya uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita uliofanywa wakati wa mzozo wa mwaka 2013 na mwaka 2014 kati ya waasi wa zamani wa Seleka na anti-balaka, kundi la wanamgambo ambalo watuhumiwa hao wawili walikuwa viongozi.

Wakati wa kusikilizwa kwa kesi hii ambayo inaanza Alhamisi hii, suala la mwendesha mashtaka litakuwa kuwashawishi majaji kuwafungulia mashtaka watuhumiwa hao wawili. Kwa sababu watu hao wawili bado hawajashtakiwa: kesi hii inalenga kuthibitisha au la mashtaka dhidi yao.

Patrice Ngaissona, ambaye anachukuliwa kama kiongozi wa juu wa kundi la Wanamgambo wa Anti-balaka, alikamatwa nchini Ufaransa mnamo mwezi Desemba 2018 na kumkuta Alfred Yekatom wiki chache baadaye katika gereza la ICC.

Alfred Yekatom, alikuwa mbunge na katika kikao cha Bunge la kitaifa, alitoa silaha yake ndogo aina ya bastola na kuwatishia usalama wabunge wenzake, kabla ya kujikuta gerezani na kisha kupandishwa ndege kwenda Hague mwezi Novemba 2018.

Wakati wa vita, aliongoza bataliani ya watu 3,000, kwa mujibu wa upande wa mashtaka, huku akifanya uhalifu na kuwalenga Waislamu.

Kiongozi wa zamani wa kundi la wanamgambo la Anti-balaka, Alfred Yekatom Rombhot, maarufu "Rambo", akifikishwa kwa mara ya kwanza mbele ya Mahakam ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) Ijumaa, Desemba 23, 2018.
Kiongozi wa zamani wa kundi la wanamgambo la Anti-balaka, Alfred Yekatom Rombhot, maarufu "Rambo", akifikishwa kwa mara ya kwanza mbele ya Mahakam ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) Ijumaa, Desemba 23, 2018. © REUTERS/Piroschka van de Wouw/Pool

Washukiwa hao wawili ni raia wa kwanza kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati kufikishwa mbele ya Mahakam ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC). Lakini uMwendesha mashtaka anaendelea na uchunguzi uliofunguliwa mwaka 2014 kwa ombi la serikali ya Bangui. Mwisho wa kesi hii, uliopangwa tarehe 27 Septemba, majaji watakuwa na siku 60 kutoa uamuzi wao.

Mamlaka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati imevitaka vyombo vya habari vya serikali kurusha hewani moja kwa moja kesi hii. Njia mojawapo ya kuwawezesha raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati kuelewa vizuri kilichotokea na kuelekea kwenye njia ya kuboresha maridhiano, amebaini msemaji wa serikali Ange-Maxime Kazagui,

"Tunangojea mashtaka yawe wazi na kwa raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, wale wanaosubiri ukweli na haki, waweze kufidiwa. Tunataka raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati waweze kusikia, kutazama, kufahamishwa. Kulitokea nini? Je! Ni kweli wana hatia? Walifanya nini? Ni wao tu ndio nahusika na makosa hayo? Ni njia ya kuelekea kuelewa kile kilichotokea kwa raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati. Kwa hivyo ni juhudi kuelekea amani. "

Hata hivyo waziri huyo amesema kuwa kwa sasa ni kundi la anti-balaka ambalo linashughulikiwa kupitia watu hao wawili. Kundi la waasi la zamani la Seleka bado halijafikishwa mbele ya Mahakama ya Kimtaifa ya Uhalifu wa Kivita kujibu tuhuma dhidi yake.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.