Pata taarifa kuu
TUNISIA-SIASA-USALAMA

Rais wa zamani wa Tunisia Zine el-Abidine Ben Ali aaga dunia

Zine el-Abidine Ben Ali, rais wa zamani wa Tunisia (1987-2011), amefariki dunia. Aliapishwa mnamo Novemba 12, 2009, mbele ya Bunge la Tunisia, kwa kuchaguliwa kwake kama rais kwa muhula wa tano.
Zine el-Abidine Ben Ali, rais wa zamani wa Tunisia (1987-2011), amefariki dunia. Aliapishwa mnamo Novemba 12, 2009, mbele ya Bunge la Tunisia, kwa kuchaguliwa kwake kama rais kwa muhula wa tano. FETHI BELAID/AFP

Rais wa zamani wa Tunisia Zine el-Abidine Ben Ali amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 83, wakili wake amesema leo Alhamisi. Baada ya mihula mitano katika uongozi wa nchi, Ben Ali alilazimika kuondoka madarakani kufuatia kuzuka kwa maandamano makubwa.

Matangazo ya kibiashara

Ben Ali alikuwa anaishi uhamishoni nchini Saudi Arabia tangu kuanguka kwa utawala wake mnamo mwaka 2011.

Zine el-Abidine Ben Ali ambaye raia wengi wa Tunisia wanamfahamu kwa jina la "Benavie" amefariki dunia. Rais wa zamani wa Jamhuri ya Tunisia, Zine el-Abidine Ben Ali, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 83, wakili wake ametangaza leo Alhamisi, Septemba 19 .

Tangu mwaka 2011, kiongozi huyo wa zamani alikuwa amekimbilia Jeddah, kwenye mwambao wa Bahari Nyeusi, nchini Saudi Arabia, pamoja na baadhi ya watu wa familia yake, kufuatia maandamano ya raia yaliyozuka katika baadhi ya nchi za Kiarabu. Baada ya kutawala Tunisia tangu mwaka 1987 hadi mwaka 2011, Ben Ali alilazimika kuondoka madarakani Januari 14 mwaka 2011, na kuachia raia wenye nia ya kufanya mabadiliko na kutetea uhuru na kuinua "uchumi wa Tunisia" ambao ulikuwa umedorora.

Mnamo mwaka 2018, baada ya kesi kadhaa ambazo hakuripoti, Ben Ali alihukumiwa kifungo cha zaidi ya miaka 200 jelakwa mashtaka mbali mbali ikiwa ni pamoja na mauaji, uporaji, ufisadi mateso.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.