Pata taarifa kuu
MUGABE-ZIMBABWE-SIASA-MAZISHI

Mugabe sasa kuzikwa katika kijiji alichozaliwa

Wanajeshi wakiwa wameubeba mwili wa rais wa zamani wa Zimbabwe  Robert Mugabe  tarehe 13 mwezi Septemba 2019
Wanajeshi wakiwa wameubeba mwili wa rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe tarehe 13 mwezi Septemba 2019 ®REUTERS/Siphiwe Sibeko

Rais wa zamani wa Zimbabwe sasa atazikwa katika kijiji alichozaliwa katika eneo la Zvimba,, hii ikiwa ni awamu nyingine ya mvutano kati ya familia na serikali ni wapi kiongozi huyo azikwe.

Matangazo ya kibiashara

Awali, serikali ilikuwa imesema Mugabe aliyefariki dunia mapema mwezi Septemba  akiwa na umri wa miaka 95 akiwa nchini Singapore, angezikwa katika makaburi ya mashujaa jijini Harare.

Uamuzi wa serikali ulikubaliwa na Familia, lakini hilo limebadilika na haijawa wazi ni kwanini serikali ya Zimbabwe imefanya mabadiliko haya.

Hata hivyo, Waziri wa Habari nchini humo Nick Mangwana katika taarifa yake amesema, serikali imeona ni vema itii matamanio ya familia kuhusu ni wapi mpendwa wao azikwe.

Mwezi huu kulikuwa na ibada ya kumbumbuka Mugabe iliyofanyika jijini Harare na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka barani Afrika.

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.