Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-SIASA

Kiongozi wa upinzani mweusi ajiuzulu kwenye chama cha AD Afrika Kusini

Kiongozi wa upinzani, kiongozi wa chama cha Democratic Alliance, Mmusi Maimane kwenye mkutano wa hadhara Pretoria.
Kiongozi wa upinzani, kiongozi wa chama cha Democratic Alliance, Mmusi Maimane kwenye mkutano wa hadhara Pretoria. © GULSHAN KHAN / AFP

Kiongozi mweusi wa chama kikuu cha upinzani nchini Afrika Kusini ametangaza kujiuzulu kwenye uongozi wa chama chake, cha Democratic Alliance. Kujiuzulu kwake kunajiri siku tatu baada ya Herman Mashaba kujiuzulu kutoka chama hicho na pia kama meya wa mji wa Johannesburg.

Matangazo ya kibiashara

Mmusi Maimane ni mweusi wa kwanza kuongoza chama hicho, kwa muda mrefu kilichukuliwa kama chama cha Wazungu.

Chini ya uongozi wake, chama cha Democratic Alliance kilipata ushindi wa kihistoria katika uchaguzi serikali za mitaa miaka mitatu iliyopita.

Lakini chama hicho kinaendelea kugawanyika kati ya chama chenye itikadi ya mageuzi na chama kihafidhina.

Wengi hawakushangazwa na hatua hii ya kujiuzulu kwa Mmusi Maimane. Alikuwa ameweka usawa wa kikabila kwenye sera yake na alifanya kazi kwa kwa kuwashawishi watu weusi walio wengi nchini Afrika Kusini kujiunga na chama chake.

Mmusi Maimane amejiuzulu kufuatia mzozo unaotokana na ubaguzi wa rangi ndani ya chama chake Democratic Alliance.

Mmusi Maimane amesema chama hicho hakiweza tena kuwa chombo stahiki kwa malengo yake ya kuwepo taifa lenye umoja.

Maimane ameeleza kwamba alipata tabu katika kukifanya chama hicho ambacho kwa muda mrefu kimekuwa na wafuasi weupe wa kiberali - kuwavutia wapiga kura weusi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.