Pata taarifa kuu
URUSI-AFRIKA-USHIRIKIANO

Vladimir Putin: Nataka kuzidisha mara mbili biashara kati ya Urusi na Afrika

Rais wa Urusi Vladimir Putin na Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sissi kwenye Mkutano kati ya Urusi na Afrika Sochi, Oktoba 23, 2019.
Rais wa Urusi Vladimir Putin na Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sissi kwenye Mkutano kati ya Urusi na Afrika Sochi, Oktoba 23, 2019. Sputnik/Mikhail Metzel/Kremlin via REUTERS

Mkutano wa siku mbili kati ya Urusi na Afrika, unamalizika leo mjini Sochi. Viongozi wengi kutoka Afrika wana matumaini kuwa ushirikiano katika sekta mbalimbali kati ya Urusi na Afrika utaongezeka baada ya mkutano huo.

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatano, rais Vladimir katika mkutano huo wa kwanza na viongozi zaidi ya 30 wa Afrika, alitanagza kuwa nchi yake itaongezeka kiwango cha uwekezaji barani Afrika hasa katika masuala ya usalama na miradi ya nyuklia nchini Nigeria na Rwanda.

Wakati wa hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa kilele wa siku mbili kati ya Urusi na Afrika Rais Vlamidir Putin alisema kuwa inawezakana kuongeza maradufu thamani ya biashara kati ya Urusi na Afrika katika kipindi cha miaka minne au mitano inayokuja.

Biashara kati ya pande hizo mbili tayari imeongezeka maradufu katika kipindi cha maika mitano na kufikia thamani ya dola bilioni 20 za Marekani, kiwango ambacho Putin amekitaja kuwa kidogo

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustine Archange Toudera amemwambia rais Putin, kuwa kuongeza zaidi msaada wa kijeshi nchini mwake itakusaidia katika vita dhidi ya waasi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.