Pata taarifa kuu
URUSI-AFRIKA-USHIRIKIANO

Swala la msaada wa Urusi katika vita dhidi ya ugaidi barani Afrika lajadiliwa Sochi

Mkutano wa kilele wa Sochi kati ya Urusi na Afrika ulimalizika Alhamisi, Oktoba 24.
Mkutano wa kilele wa Sochi kati ya Urusi na Afrika ulimalizika Alhamisi, Oktoba 24. © Sergei Chirikov/Pool via REUTERS

Kama mkutano wa kilele wa Sochi, uliomalizika Alhamisi (Oktoba 24), ulilenga maswala ya kiuchumi, Vladimir Putin na viongozi wa Kiafrika pia wamejadili changamoto za vita dhidi ya ugaidi barani Afrika na msaada wa Moscow kwa wakuu wa bara la Afrika, haswa katika eneo la Saheli au mzozo wa Libya.

Matangazo ya kibiashara

Tangu mwaka 2017, Urusi imetia saini mikataba ya ushirikiano wa kijeshi na nchi 20 za Afrika. Na inatarajia kuendelea katika mwelekeo huo.

Vladimir Putin anataka kuonekana kama msaada unaowezekana katika vita dhidi ya ugaidi katika bara hilo na kuzuia majaribio yoyote ya mapinduzi ya serikali za Kiafrika. Hayo aliyaweka wazi jana Alhamisi katika kikao cha mjini Sochi.

"Ugaidi, kuenea kwa itikadi kali, uhalifu wa mipakani, na uharamia huzuia maendeleo ya bara la Afrika. Nchi kadhaa zinakabiliwa na hali ya maandamano iliyotokea katika nchi za Kiarabu. Matokeo: Afrika yote ya Kaskazini inakabiliwa na mdororo wa usalama ... Katika kanda hiyo, lakini pia katika maeneo ya Sahara na Sahel, katika Jimbo la Ziwa Chad, kunapatikana makundi mengi ya kigaidi yakiwemo Islamic State, al-Qaeda, Boko Haram na al-Shebab. Ndio sababu tunaamini kuwa ni muhimu kuongeza juhudi za pamoja za Urusi na Afrika katika vita dhidi ya ugaidi," amesema Vladimir Putin.

Rais wa Urusi anataka "kuimarisha ushirikiano kati ya vikosi vya usalama na idara maalum za Urusi na nchi za Afrika", akisisitiza kuhusu ujuzi na mafunzo.

"Tunahitaji kuratibu juhudi zetu na kuanzisha zoezi la kubadilishana taarifa. Tunatamani kutoa mafunzo, katika siku zijazo, kwa vikosi vya usalama vya Afrika katika taasisi za elimu maalum za Urusi. Kwa sasa, katika shule za juu za Wizara ya Ulinzi ya Urusi, wanajeshi wa nchi ishirini kutoka Afrika wanasoma, " Rais Putin ameongeza.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.