Pata taarifa kuu
CHAD-USALAMA

Maafisa watatu wa Wizara ya Afya watekwa nyara karibu na Ziwa Chad

Ziwa Chad katika mkoa wa Bol, mji mkuu wa Jimbo la Ziwa.
Ziwa Chad katika mkoa wa Bol, mji mkuu wa Jimbo la Ziwa. © SIA KAMBOU / AFP

Maafisa watatu wa Wizara ya Afya nchini Chad wanashikiliwa mateka tangu Jumatano, Oktoba 30. Maafisa hao walitekwa nyara na watu wasiojulikana kati ya Ngouboua na Chukutalia, vijiji viwili vya Jimbo la Ziwa Chad.

Matangazo ya kibiashara

Walikuwa wakirudi kutoka kwa ziara ya kikazi na walitekwa na watu hao waliojihami kwa bunduki na kuwapeleka sehemu isiyojulikana.

Gari ndogo lililowasafirisha watu hao watatu limepatikana kwenye barabara inayotoka Ngouboua kwenda Chuktalia, kwenye mwambao wa kaskazini mwa Ziwa Chad.

Kulingana na ripoti ya awali, gari hilo ambalo lilikuwa limemsafirisha afisa Mkuu wa Afya katika Wilaya ya Baga Sola, muuguzi na dereva wao, lilizuiliwa na watu wenye silaha kisha kuwateka nya waliokuwemo na kuwapeleka, wakitumia mitumbwi ya wavuvi kwenye Ziwa Chad.

Chanzo hicho kinabaini kwamba kundi la Boko Haram lina kambi za mafunzo kwenye visiwa vingi vya Ziwa Chad ambapo inashukiwa kuwa mateka hao wamepelekwa.

Kulingana na wachambuzi kadhaa, hii ni mara ya kwanza wapiganaji wa Boko Haram kufanya kile kinachoonekana kama utekaji nyara wa wafanyakazi wa afya ambao ni raia wa kawaida.

Kawaida, Boko Haram huteka nyara wasichana na wanawake baada ya mashambulizi yao.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.